(Sung in Swahili)

Refrain:
Usisahau ulikotoka, mama eh (Mother do not forget from whence you came from)
Usisahau ulikotoka, baba eh (Father do not forget from whence you came from)
Iko faida kunyenyekea, mama eh (There’s value in humility)
Unyenyekevu hauna hasara, baba eh (Being humble has no loss)

Neno la Mungu linasema (The Word of God says)
Neno la Mungu limeweka wazi (The Word of God has made it evident)
Huwainua wanyenyekevu (It lifts the humble)
Na huwashusha wenye kiburi (And lowers the proud)
Ulimwomba Mungu kwa uchungu mwingi (You prayed to God in pain)
Leo amekusaidia umefanikiwa (Today He has blessed You to success)
Usisahau ulikotota mama we (Do do not forget from whence you came from)
Usisahau wale waliokusaidia (Do not forget those who helped you)

Ni kweli umesoma sana (It’s true you have studied far)
Ni kweli una kazi nzuri (It’s true that you have a good job)
Ni kweli una kipaji kizuri sana (It’s true that you have a good talent)
Lakini usisahau ulikotoka (But do not forget from where you came from)
Usisahau wale waliokushika mkono (Do not forget those who held your hand)
Usisahau wale walioomba kwa ajili yako (Do not forget those who prayed on your behalf)
Usisahau ulikotoka mama we (Mother, do not forget where you came from)

(Refrain)

Ninawakumbuka wale wakoma kumi (I remember the ten lepers)
Walioponywa na Bwana Yesu (That were healed by Jesus)
Ni mmoja tu alirudi kushukuru (It is only one who came back to give thanks)
Ndipo muujiza wake ukawa wa kudumu (That is why his miracle lasted)
Ni kweli uko busy sana (It’s true that you are busy)
Ni kweli wewe ni mtu mzito sana (It’s true that you are an important person)
Ni kweli unaonwa kwa appointment (It’s true that you are seen by appointment)
Ni kweli umeinuliwa sana (It is true that you are lifted up)
Lakini usisahau ulikotoka (But do not forget from where you came from)
Usisahau yale maombi uliyoomba (Do not forget the prayers you prayed)
Usisahau nadhiri zile ulizoweka (Do not forget the vows you placed)
Usisahau kumshukuru Mungu wako (Do not forget to give thanks to Your God)

Ni kweli umefanikiwa sana (It is true that you are successful)
Dada ni kweli wewe ni mrembo sana (My sister, it is true that you are very beautiful)
Ni kweli umesoma sana (It is true that you have studied a lot)
Usisahau ndugu zako kijijini (Do not forget your brothers in the village)
Usisahau wazazi walikusomesha kwa shida (Do not forget your parents schooled you in difficulty)
Iko faida kushukuru Baba we (There is value in thanking the Fatehr)
Muujiza wako utadumu (That your miracle may last)

(Refrain)

Mungu hutumia watu kuwainua watu (God uses people to lift others)
Usisahau watu ambao Mungu amewatumia kwenye maisha yako (Do not forget those that God has used in your life)
Kukufikisha hapo ulipo (To get you where you are today)
Iko faida kuwakuwakumbuka (There is value in remembering them)
Iko faida kumshukuru Mungu (There is value in thanking God)
Kwa hapo alipokufikisha (For where he has gotten you)