(Sung in Swahili)

Ya nini Mungu kujificha wakati wa shida?
(God, why do you hide from me in times of trouble?)
Wakati mwingine kama kweli huoni
(Other times it is like You do not see)
Wajua yote yalonikuta hasim’liki
(You know all that have happened to me that cannot be said)
Nimelia na kujinyamazisha pekee yangu
(I have cried and comforted myself)

Moyoni nikataabika, Furaha ikaenda
(My heart struggled, my joy fled)
Sikumwona wa kumwelezea shida
(I did not see anyone to confide with my troubles)
Rafiki pekee namwamini, ni Yesu mfariji
(The only friend I trust is Jesus the Comforter)
Ndio maana sijamwambia mtu shida zangu
(This is why I have not told people of my troubles)

Refrain:
N’tasubiri na kusubiri sitachoka
(I shall wait and wait without tiring)
Nimeshamezana na wewe kwa maombi
(I have already spoken to You in prayers)
Us’pojibu, au ujibu n’taelewa
(Whether You answer or not, I shall understand)
Nash’kuru, hata kwa majaribu
(I am thankful even in my trials)
Mungu unasababu (God You have a reason)
Mimi kuishi maisha kama haya
(For me to live such a life) (Repeat)

Kwa nini sasa umesimama mbali nami Bwana?
(Why do You stand away from me Lord?)
M’da mwingi mi najihisi mi ni mpweke
(A lot of times I feel lonely)
Jidhihirishe mi nikuone, nakuhitaji Bwana
(Manifest Yourself, let me see You, Lord I need You)
Nibariki sasa ukijibu maombi, yangu
(Bless me now as You answer my prayers)
Najua mengi nimekuudhi, nimetenda dhambi
(I know I have angered You, I have sinned)
Ndio maana ukasimama mbali nami
(That is why You’ve distanced Yourself from me)
N’samehe yote yote bure, kwa damu ya Yesu
(Forgive me all of it, freely, in the Blood of Jesus)
Nifanye mi ni we mtoto wako siku, zote
(Make me Your child, forever)

(Refrain)