(Sung in Swahili)

Hainidhuru kama nasafiri kwenye bahari (I’m not harmed though I sail)
Ya mawimbi kwani Yesu ni nahodha wangu (On stormy seas, for Jesus is my captain)
Atanifikisha bandarini (He will guide me safely to the harbor)
Japo misukosuko yaniandama (Though troubles follow me)
Hainidhuru kwani nahodha yuko kwenye chombo (They do not harm me, for the pilot is in the ship)
Sikatai, kodi ya nyumba nimekosa (I do not deny that I do not have any money for rent)
Na watoto, ada shuleni walifukuzwa (The children were sent from school for lack of fees)
Na maadui wakiongezeka wakinijia (Though my enemies increase in number)
Bado hainidhuru, nitakuwa salama (I am not harmed, I shall be safe)

Najua niko doro mfuko wangu zero, hainidhuru bado (I know I no purpose and money; but I am not harmed)
Bado nazichangachanga pesa, mambo yatakuwa sawa (I am still struggling to raise money, it shall be well)
Usiku ukiwa mrefu, asubuhi yaja (Though the night is long, dawn arrives)
Shida hazikwamishi safari yangu (Troubles do not hinder my way)
Ushindi wangu uko mbele yangu, naamini (I believe that my victory is ahead of me)

Refrain:
Repeat: Bado, bado hainidhuru (Yet I will not be harmed)
Japo shida nyingi zinanikumba (Though I encounter many troubles)
Matatizo mengi natahadhika (Many problems follow me)
Nahodha wangu Yesu, yuko kwenye chombo (My pilot Jesus, is on duty)
Ananiongoza, atanifikisha (He leads me, he will get me there)

Ingawa ni jioni, lazima nifike kule (Though it is night, I shall arrive there)
Yesu mtuliza barahi atanifikisha kule (Jesus the calmer of seas will get me there)
Baraka zangu lazima nishike nimiliki mie (I must claim my blessings)
Sivurugwi, nasema sitishwi (I am not troubled, I am not disturbed)
Kwa mateso sivurugwi, kwa kelele bado sitishwi (I am not disturbed by troubles and shouts)

Kwa giza ije mishale, ije mateso yaje, potelea mbali (Though arrows and troubles come by night)
Magonjwa nayo kusongwa sana havitabadilisha, ukweli wa mambo (Though sickness and troubles come, they’ll change nothing)
Sivurugwi, na tena sitishwi (I am neither troubled nor distrurbed)
Kwa mateso sivurugwi, kwa kelele tena sitishwi ( am not disturbed by troubles and shouts)

Namwamini namwamini, Mungu wa ajabu (For I believe the Awesome God)
Ananipeleka, ananipeleka, Eh Kanani (The one who will guide me unto Caanan) (Repeat)

(Refrain)

Advertisement