Sikuachi Tena (I Won’t Leave You Again) Lyrics by Zabron Singers

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Tunaishi kwa nguvu ya Mungu, Ye ndo katuweka hapa
(We live by God’s Power, He placed us here)
Kila hatua tunapitia, ye ndiye mlinzi wetu
(He guards all the steps we take)
Asubuhi ifikapo, hujua siku itaenda vipi
(When morning comes, he knows how the day will go)
Je n’tavuka salama, mchana jioni hata usiku
(Will I cross safely the, morning, evening and night?)
Kwa dakika,sekunde hujua siku itaenda vipi
(By minutes and seconds, he knows how the day will go)
Kupata na kokosa, ajua mimi n’tapata nini
(Receiving and Losing, He knows what I will get)
Kulala, kuamka, ajua mi n’taamka vipi
(Sleeping, and rising, he knows how I will wake)
Maisha yetu yote, Mungu ndiye anazo siri zetu
(The Lord knows the secret of all our lives)

Refrain:
We ni Mungu wangu, sikuachi tena
(You are my God, I will not leave You again)
Nikuwepo leo ni rehema zako zaniwezesha
(Me being here today, is through Your Mercies)
Sina haki mimi, kujisifu tena
(I do not have the right to boast of myself)
Kwani bila wewe hakika mimi singekuwa hivi
(For Without You, truly I would not be this way) (Repeat)

Mwanga wangu wa njia na nyota katika maisha yangu
(The Light to my path and the Star in my life)
Ye ni Mungu wa nuru, ushindi hata vitu vyote vyake
(He is the God of light, victory and all things are His)
Upatacho shukuru, ni Mungu ndiye kakuweka hapo
(Be thankful for what you get, it is God who placed you there)
Usisahau kumtumikia bado ungali hai
(Do not forget to serve Him, while you are still alive)

Kumbuka kuna siku utadaiwa kwa matendo yako
(Remember there is a day you will give account for your actions)
Iwe jema, kwa baya, watu pia umewatenda vipi?
(For good or for ill, How have you treated others?)
Je wazitumiaje baraka ulizopewa na Mungu?
(How are you using the blessings you were given by God?)
Suluhisho pekee, ni Mungu tumpe maisha yetu
(The only solution, is to give God our lives)

(Refrain)

Nitasubiri (I Will Wait) Lyrics by Zabron Singers

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Ya nini Mungu kujificha wakati wa shida?
(God, why do you hide from me in times of trouble?)
Wakati mwingine kama kweli huoni
(Other times it is like You do not see)
Wajua yote yalonikuta hasim’liki
(You know all that have happened to me that cannot be said)
Nimelia na kujinyamazisha pekee yangu
(I have cried and comforted myself)

Moyoni nikataabika, Furaha ikaenda
(My heart struggled, my joy fled)
Sikumwona wa kumwelezea shida
(I did not see anyone to confide with my troubles)
Rafiki pekee namwamini, ni Yesu mfariji
(The only friend I trust is Jesus the Comforter)
Ndio maana sijamwambia mtu shida zangu
(This is why I have not told people of my troubles)

Refrain:
N’tasubiri na kusubiri sitachoka
(I shall wait and wait without tiring)
Nimeshamezana na wewe kwa maombi
(I have already spoken to You in prayers)
Us’pojibu, au ujibu n’taelewa
(Whether You answer or not, I shall understand)
Nash’kuru, hata kwa majaribu
(I am thankful even in my trials)
Mungu unasababu (God You have a reason)
Mimi kuishi maisha kama haya
(For me to live such a life) (Repeat)

Kwa nini sasa umesimama mbali nami Bwana?
(Why do You stand away from me Lord?)
M’da mwingi mi najihisi mi ni mpweke
(A lot of times I feel lonely)
Jidhihirishe mi nikuone, nakuhitaji Bwana
(Manifest Yourself, let me see You, Lord I need You)
Nibariki sasa ukijibu maombi, yangu
(Bless me now as You answer my prayers)
Najua mengi nimekuudhi, nimetenda dhambi
(I know I have angered You, I have sinned)
Ndio maana ukasimama mbali nami
(That is why You’ve distanced Yourself from me)
N’samehe yote yote bure, kwa damu ya Yesu
(Forgive me all of it, freely, in the Blood of Jesus)
Nifanye mi ni we mtoto wako siku, zote
(Make me Your child, forever)

(Refrain)

Mkono Wa Bwana (The Hand of God) Lyrics by Zabron Singers

1 Comment


(Sung in Swahili)

Mengi mazuri tumeyaona, Mungu umetenda (God, We have witness Your Good works)
Ni kweli we muweza (Truly You are able)
Ulitamka vitu vikawa (By your Word the world came to be)
Neno tu latosha (Your word is enough)
Ukisema umetenda (What You say, You have done)
Bahari shamu Isiraeli (The Isralites at the Red Sea)
Ah uliwavusha (You helped them to cross)
Kawatoa utumwani (You rescued them from slavery)
Watumishi wako umewapa (You have granted Your servants)
Yote waombayo (All they have prayed for)
Ikiwa umependezwa (If you are pleased)

Uamulo hakuna wa kulipinga (None can gainsay your Word)
Hakika we ni Mungu, wa vyote (Truly You are God, over all)
Unatawala dunia na vilivyomo (You rule over earth and all in it)
Makuu umeyatenda, Jehova (You have done great things, Lord)

Refrain:
Tumeuna, mkono wako Bwana (Lord we have seen Your hand)
Matendo yako Bwana ni makuu mno (Your work are great)
Umetutoa mbali, ukatushika mkono (You have brought us from far, holding our hands)
Mahali uliona pekee hatuwezi (Where You saw we couldn’t by ourselves)
Chini hata juu, watu unawainua (From the lowest to the highest, You lift people)
Sifa na utukufu ni zako milele (Praise and Glory belong to You forever)
Twasifu jina lako, milele tutakusifu (We will praise Your name forever )
Daima we umwema tutaishi kwako (Forever You are Good, we shall dwell with You)
(Repeat)

Ona x? (Witness)
Msalabani ulitufia, hm ulitupenda (You died on the cross, for You loved us)
Dhambi zetu ukabeba (You carried our sins)
Baraka zako tuliziomba kweli tumeona (The blessings we prayed for, we have seen)
Hakika unabariki (Truly You bless)
Hata vipaji we ndo hutoa umetuwezesha (You are the one who give talents)
Tunaimba na kusifu (We sing and praise)
Walio haki hutowaacha, uliwaahidi (You promise not to leave the righteous)
Hata mwisho wa dahari (Even until the end of the world)

Hm watu wako umewapa mamlaka (You have given Your people authority)
kwa jina lako Yesu (In Your Name, Jesus)
Waponye (To heal)
Na huna ubaguzi (You do not discriminate)
Wote ni sawa kwako (All are equal before You)
Umetuita Yesu, tupone (You have called us Jesus, to heal)

(Refrain)

Ona x? (Witness)
Daima we umwema tutaishi kwako (Forever we shall dwell with You)
(Repeat)

%d bloggers like this: