Minyororo (Chains) lyrics by Esther Wahome

Leave a comment


Miguu na mikono umefungwa, Mawazo yako yamefungwa
Macho umefungwa hauoni,Roho yako pia imefungwa
Yesu ana ufunguo, usife moyo

Jela ya shetani, minyororo minyororo
Yesu afungua minyororo minyororo
Jela ya shetani, minyororo minyororo
Yesu afungua minyororo minyororo

Njaa na kiu kwenye jela, Mateso mengi ya kutisha
Wewe mtupu hauna kitu,Magonjwa pia yamekusonga
Yesu ana ufunguo wa huo jela

Mpango wa shetani kwenya jela,Ni kuiba tena na kuharibu
Mshahara wake yeye ni mauti, Kubali Yesu yeye akuweke huru
Akutoe jela ya shetani

Jela ya shetani, minyororo minyororo
Yesu afungua minyororo minyororo
Jela ya shetani, minyororo minyororo
Yesu afungua minyororo minyororo

Wazee tokeni hiyo jela, wamama tokeni hiyo jela
Vijana tokeni hiyo jela, watoto tokeni hiyo jela
Jela ya hukumu, jela ya mauti

Jela ya shetani, minyororo minyororo
Yesu afungua minyororo minyororo
Jela ya shetani, minyororo minyororo
Yesu afungua minyororo minyororo

Hachagui (He Does Not Discriminate) Lyrics by Esther Wahome

Leave a comment


Chorus:
Hachagui kabila, hachagui taifa
Hachagui tajiri, wote awapenda
Hachagu kabila, hachagui taifa
Hachagui tajiri, wote awapenda

Nilisikia kuna mpenzi ambaye hachagui
wote awapenda, wote awajali
Nilimpa maisha yangu nayo yakawa sawa
Ni mwanaume wa wanaume, hachagui hachagui

(Chorus)

Nilianza safari kwa mataifa mbalimbali
Ili nitangaze yesu na matendo yake
Wamekubali wamesema yesu ni namba moja
Ni mwanaume wa wanaume, hachagui hachagui

(Chorus)

Natangazia wazee pia na vijana
Kwani huyu mpenzi, hachagui miaka
Hata watoto anasema, wote waje kwake
Ni mwanaume wa wanaume, hachagui hachagui

(Chorus)

Nampenda huyu mpenzi aliyenipenda mbele
Tena alijitoa afe kwa ajili yangu
Damu yake alimwaga ili nisipotee
Ni mwanaume wa wanaume,

(Chorus)

Natangaza hachagui, huyu yesu awapenda eh oh
Awapenda wote, huyu yesu
Awajali wote, haleluyah
Awajali wote

(Chorus)

Daktari lyrics by Esther Wahome

Leave a comment


Daktari wa moyo nipima pime, Daktari wa mwili wangu touch me
Daktari wa moyo nipima pime, Daktari wa mwili wangu touch me

Nimeskia sifa zako daktari,Vile Sara na Hana uliwapa wana
Ukimgusa tasa anapata mapacha, Oh Daktrari, oh Daktari
Oh daktari, daktari touch me!

Daktari wa moyo nipima pime, Daktari wa mwili wangu touch me
Daktari wa moyo nipima pime, Daktari wa mwili wangu touch me

Kuna vile unaelewa unyonge wangu, au uchungu wangu na haja zangu
Hata na akili zangu dhamiri yangu, Tafadhali daktari
Oh daktari,Eh daktari, daktari touch me!

Daktari wa moyo nipima pime, Daktari wa mwili wangu touch me
Daktari wa moyo nipima pime, Daktari wa mwili wangu touch me

Wazee wamama na vijana wapime oh, hata watoto pia uwapime baba
Ukipata magonjwa, uwatibu daddy, moyo mwili na moyo wewe ni daktari
Eh Daktari, daktari, oh daktari, daktari

Daktari wa moyo nipima pime, Daktari wa mwili wangu touch me
Daktari wa moyo nipima pime, Daktari wa mwili wangu touch me

Chakutumaini Sina (My Hope is Built on Nothing Less) Hymn Lyrics by Martha (Tenzi 15)

6 Comments


(Sung in Swahili)

Note: The translation is not a direct one, as the song was translated from English to begin with. But no meaning is lost/exaggerated in attaching the formal English translation.

uuhh Chakutumaini, mimi sina, ila hiyo damu
(My hope is built on nothing less, Than Jesus’ blood)

Chakutumaini sina (My hope is built on nothing less)
Ila damu yake Bwana (Than Jesus’ blood and righteousness)
Sina wema wa kutosha (I dare not trust the sweetest frame)
Dhambi zangu kuziosha (But wholly lean on Jesus’ name)

Chorus:
Kwake Yesu nasimama (On Christ, the solid Rock, I stand)
Ndiye mwamba ni salama (All other ground is sinking sand)
Ndiye mwamba ni salama (All other ground is sinking sand)
Ndiye mwamba ni salama (All other ground is sinking sand)

Njia yangu iwe ndefu (When darkness veils His lovely face)
Ye hunipa wokovu (I rest on His unchanging grace;)
Mawimbi yakinipiga (In every high and stormy gale)
Nguvu ndizo nanga (My anchor holds within the veil)

(Chorus)

Nikiitwa hukumuni (When He shall come with trumpet sound)
Rohoni nina amani (Oh, may I then in Him be found)
Nikivikwa haki yake (Dressed in His righteousness alone)
Sina hofu mbele zake (Faultless to stand before the throne)

(Chorus)

Damu yako na ahadi (Your promises and blood)
Nategemea daima (Support me in the whelming flood)
Yote chini yakiisha (When all around my soul gives way)
Mwokozi atanitosha (He then is all my hope and stay)

(Chorus)

(Verse 1)

(Chorus)

Sitanyamaza Lyrics by Rose Muhando

2 Comments


(Sung in Swahili)
Eeeehhhh…. Mimi Mungu (Me, God)
Matendo nitalia, Kwa sinani nitaomboleza
Sodoma nitanung’unika, Mipakani nitashambulia
Mijini wameniacha,Kila mara nitashambulia
Maisha ya wanadamu, Yamenichosha….

Oh oh mimi
Sitanyamaza, wala sitanyamaza
Lakini nitalipa ujira wa vifuani mwao
Maovu yenu ninyi, pamoja na baba zenu
nasema nitalipa ndio mjue mimi ni Bwana
Mmefukiza uvumba, na kunitukana
Kwa ajili ya haya mtajutia vitani mwenu?(repeat)

mmefanya uzinzi katikati ya milima
Usiku wa manane mmefanya ukahaba
Kwenye njia kuu na vichochoro mmefanya mapatano
Kwenye mialoni na mipera mmefanya machukizo (repeat)

Ulitumaini uzuri wako ukafanya ukahaba
Kila kijana aliyepita ulimwona anafaa
Awe mzuri na sura mbaya ulifunua marinda

Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi mapenzi zako mbona sasa unakonda
Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi waelizamu (?) wako mbona sasa unakonda

Miji mizuri imekuwa ukiwa
Majumba mazuri yamefungwa kabisa
Wana wa wana wamebaki yatima
Kiburi chamuwamu(?) imekoma kabisa (repeat)

Hebu sasa piga kelele uliye kahaba,
Shika kinubi omboleza upate kukumbukwa (repeat)

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye
Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)

Lakini Bwana asema hivi, nitawaponya
Yeye mwenyewe aahidi, nitawabariki
Mimi ni alfa na omega, mwanzo na mwisho
Jamani mimi ni mungu, mwingine hapana

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)

Older Entries Newer Entries