Nina imani, siku za mateso zitapita (I have faith that troubled days will be over)
Nina imani, siku ya kutoka ghetto, itafika (I have faith that my ghetto days will end)
Nitapata mabawa, nitapaa (I will get wings, I will fly)
Nyota itaangaza, nitang’aa (The star will light, I will shine)
Ninayotamani moyoni, nitapata (I will be granted my heart’s wishes)
No no no no, sitasahau (No no no no, I shall not forget)
Refrain:
Sitasahau, walionishikilia (I shall not forget those who held me)
Sitasahau, walioniombea (I shall not forget those who prayed for me)
Sitasahau, ni Mungu amenitendea (I shall not forget what God has done for me)
Sitasahu, sahau! (I shall not forget)(Repeat)
Nitashare-share (I will share)
Hiyo kidogo sitajiwekea (And shall not keep the little to myself)
Sitalegea-gea kushika mtu mkono (I shall not tarry to hold anyone by the hand)
Na nikiitwa somewhere, kusaidia (If I am called anywhere to help)
Hata kama sina fare, nitatembea (Even if I do not have fare, I shall not walk)(Repeat)
Oh Mfalme wa amani (Oh Prince of Peace)
Nimekaa katika mlima huu, kwa muda mrefu Mfalme (I have sat on this hill for a long time)
Sasa ninaomba Mfalme wa amani (Now I pray, Prince of Peace)
Usinipite! Usiwe mbani nami Jehova (Do not pass me by! Lord, do not be far from me)
Ninakupenda Jehova, asante (I love You Jehovah, I thank You)
Refrain:
Usinipite Bwana, usiufiche uso wako (Lord do not pass me by, do not hide Your Face)
Unapozuru watu wengine, usinipite Bwana (When You call on others, do not Pass me)
Usinitupe Bwana, usiwe mbali nami (Lord do not abandon me, be not far from me)
Unapozuru watu wengine, usinipite Bwana (When You call on others, do not pass me) (Repeat)
Watakatifu wamekusanyika, wanainama mbele zako (The holy ones are gathered, prostrate before You)
Wanasema Mtakatifu, hakuna kama Wewe (Say Oh Holy one, there is no one like You)
Twaungama na makerubi na maserafi (We confess with the Cherubim and the Seraphim)
Na wazee ishirini na wanee, wenye uhai wanne (And 24 elders, and the four beings)
Tunasema uheshimiwe, tunasema uabudiwe (Saying be glorified, be worshiped)
Tunasema uinuliwe, hakuna kama wewe (We say be lifted, there is none like You)
(Refrain)
Umesema watu wangu, walioitwa kwa Jina langu (You have said that me people, called by my name)
Wakiomba na kutubu, utasikia kutoka juu (If they pray and confess, You will listen from heaven)
Utaiponya nchi yao, utaondoa uchungu wote (You will heal their land, You shall remove all pain)
Ninaomba Masiya, usinipite Bwana (I pray Savior, do not pass me by)
Kuna wale wako vitandani, hawawezi kutembea (There are bedridden, who cannot walk)
Ninaomba Masiya, usiwapite Bwana (I pray Savior, do not pass me by)
Kuna wale wameachwa, na waume wao (There are those abandoned by their husbands)
Ninaomba Masiya, usiwapite Bwana (I pray Savior, do not pass me by)
Kuna wale wameachwa, na wake wao (There are those abandoned by their wives)
Ninaomba Masiya, usiwapite Bwana (I pray Savior, do not pass me by)
Kuna wale wameachwa na wazazi wao (There are those abandoned by their parents)
Ninaomba Masiya, usiwapite Bwana (I pray Savior, do not pass me by)
(Refrain)
Nimesikia historia yako, unainua walio chini (I have heard Your history, You lift the afflicted)
Ninaomba Masiya, usinipite Bwana (I pray Savior, do not pass me by)
Magoti yangu yamezama chini, nainua mikono yangu (My knees are sunk, I lift my hands)
Ukiniacha nitaenda wapi? Usinipite Bwana (If You abandon me, Where will I go? Do not pass me by Lord)
Uko na moyo wa huruma, uko na macho ya huruma (You are Merciful, You see with mercy)
Ninaomba Masiya, usinipite Bwana (I pray Savior, do not pass me by)
(Refrain)
Magoti yangu yamezama chini, nainua mikono yangu (My knees are sunk, I lift up my hands)
Ninasema siwezi Baba, bila wewe (I say without You Father, I cannot)
Wewe ndiwe rafiki yangu, wewe ndiwe kipenzi changu (You are my Friend, You are my Love)
Mimi sina mwingine tena, usinipite Bwana (I have no other, do not pass my by Lord)
Refrain:
Na ijulikane, wewe ni Mungu (Let it be known, that You are God)
Na ijulikane, wewe waweza (Let it be known, that You are able)
Na ijulikane watenda mambo makuu (Let it be known, that You do great things)
Na ijulikane duniani kote (Let it be known all over the world)
Niko mbele zako, miguuni mwako (I am before you, on your feet)
Nimenyenyekea nikutafute (I have humbled myself, to seek You)
Mahitaji yangu, nakuletea (My needs, I bring to You)
Mizigo yote – nakuachia (My burdens, I leave unto You) (Repeat)
(Refrain)
Ninayo imani unayaweza (I have faith that You are able)
Muweza yote, unanitosha (Omnipotent, You are enough for me)
Msaidizi wakati kama huu (A Helper in these times)
Nakuamini, nanyeyekea (I beliver in You, I humble myself) (Repeat)
Si kwa bahati mbaya uko hai leo (It is not by chance that you are alive today)
Na si kwamba wewe ni mjanja kuliko wale waliolala (It’s not that you’re cleverer than those who are asleep)
Ila yote ni muujiza wa Mungu tu (But all this, is the miracle of God)
Ni muujiza tu (It is only a miracle)
Nikilala niamke, nikiona natembea (When I sleep and then rise, when I see myself walking)
Mwenzenu, kwangu ni muujiza (Comrade, to me it is a miracle)
Asubuhi kunakucha, Jioni iikingia (When the morning dawns, and the evening arrives)
Maisha yangu, mimi ni muujiza tu (My life, I am just a miracle)
Siku ikipita, mwezi na mwaka unakwisha (The days passes, the month and the year end)
Mimi, hii kwangu ni muujiza tu (To me, all this is a miracle)
Ewe Yesu, Ee Yesu, Bwana wangu we (Jesus, Oh Jesus, Oh my Lord)
Oh kwangu ni muujiza (All this is a miracle)
Refrain:
Mimi ni muujiza, maisha yangu ni muujiza (I am a miracle, my life is a miracle)
Ee Bwana, we kwangu ni muujiza (Oh Lord, You are my miracle)
Nikilala ni muujiza, nikiamka ni muujiza (When I sleep and when I rise, it is a miracle)
Ee Bwana, we kwangu ni muujiza (Oh Lord, to me You are my miracle)
Kuna waliolala, hawakuamka (There are those who fell asleep and never rose)
Ee Bwana naona ni muujiza (Oh Lord I see all as miracles)
Walioanza safari, hawakufika (Those who started the journey, and never arrived)
Mimi leo, najiona mi muujiza (Today, I see myself as a miracle)
Kuwa hai, kutangaza neno lako (To be alive, to spread Your Word)
Bwana kwangu, mimi ni muujiza (Lord to me, I am a miracle)
Sina sababu, ya kunyamaza (I do not have a reason to be silent)
Maana kwangu, wewe Bwana ni muujiza (For to me, You Lord are a miracle)
Every day, every hour
You are faithful, to me (Repeat)
Kila siku, kila saa (Everyday, every hour)
U mwaminifu Bwana (Lord, You are Faithful) (Repeat)
Asubuhi, mchana na jioni (Morning, Afternoon and evening)
Kila majira na kila wakati, Bwana (In every Season, and every time, Lord)
U mwanifu Bwana (Lord, You are Faithful)
Unanilinda kila leo Bwana (You protect me everyday, Lord)
Uanitunza kila wakati Bwana (You preserve me all the time, Lord)
U mwaminifu Bwana (You are Faithful, Lord)