Advertisements

Shukurani (Thanksgiving) Lyrics by Goodluck Gozbert

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Ninakushukuru Mungu sababu ya mengi (God I am thankful for many things)
Hata uhai huu sikustahili (Even for the life that I did not desrve)
Ninakushukuru Mungu tena sababu ya vingi
(God I am thankful to You for many things)
Hata nikiwa nasali unajua namaanisha
(Even when I was praying, You know what I meant)
Sio kama eti nilitenda wema (It is not because I did good)
Wakuja linganisha na matendo yako makuu (That You aligned me with good things)
Mimi Mungu ningekulipa nini (What would I pay You, God?)
Ulikonitoa ni siri ya moyo (Where You got me from is my heart’s secret)
Matopeni topeni ukaniketisha na wakuu juu
(From the miry clay, You have sat me with kings)
Umenipa heshima ukanifuta machozi
(You have given me respect, You wiped my tears)
Asante oh Baba (Thank You Oh, Father)

Refrain:
Hata shukurani zangu ni kwako (Even my thanksgiving are to You)
Shukrani zangu ni kwako (My Thanksgiving are to You)
Na shukurani zangu ni kwako (My  thanks are to YOu)
Shukurani zangu ni kwako, asante Baba (My thanks to You, Thank You Father)
Aibu umefuta fedheha umefuta (You have wiped away my shame and my disgrace)
Umenipa amani, iliyo ya kweli (And have granted me true peace)
Nakumbuka nalia mimi ndo yule ambaye (I remember that I was the one that)
Nilitukanwa na kwa dharau wakasema kwisha habari yake
(I was despised and was said that my days were over)
Kuna kipindi nilikufa nikawa mifupa inayotembea
(There was a time I was dying, was a walking skeleton)
Ikiwa kwa siku za usoni walisema tunazika kesho
(They said that they would bury me tomorrow)
Ila kwa huruma uliniponya na kaburi (In Your mercy, You saved me from the grave)
Kwa huruma, ah sitosahau wema wako we Baba
(But for Your Mercy. Oh I shall not forget Your Goodness)

(Refrain)

Response: Ahsante Baba (Thank You Father)
Kama kusoma tulisoma wengi, umeniruhusu niwe na kazi nzuri
(If it’s education, we all went to school – But You have allowed me a good job)
Ajali tulipata wengi, umeruhusu nibaki na uzima
(A lot of us were in an accident, You allowed me to remain alive)
Ndoa zimefungwa nyingi, umeruhusu tubaki na amani
(A lot of marriages have been made, You have allowed us to remain peaceful)
Furaha wamekosa wengi, umeruhusu nitabasamu Baba
(A lot have no joy, You have allowed me to smile, Father)

(Refrain)

Advertisements

Nipe (Grant Me) Lyrics by Goodluck Gozbert

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Hata nikiwa sina chakula, Isinifanye kusahau (Even if I lack food, don’t let me forget)
Ulinilisha nikasaza (You fed me until I was full)
Hata nikiwa sina mavazi (Even if I have no clothing)
Isinifanye nifukuru (Do not let me blaspheme)
Na kusahau umeniweka hai (And forget you kept me alive)
Ona wapo marafiki (To see my friends )
Wanakosa kula na kuvaa (Though they lack food and clothing )
Hawalalamiki, wanakushukuru tu (They do not complain, but give thanks to You)
Mimi eh, nilikupa nini Baba (As for me, what did I give You Father)
Cha kunipa kibali (That You’ve favored me)
Kwa siku zilizofurahisha? (With days that give me joy?)

Taabu kidogo zisinifanye nikusahau (A little trouble should not let me forget)
Umeshatenda mengi – nikiwa hapa (That You’ve much that I have witnessed)
Shida itapita, bado kidogo (Troubles will pass in a little while)
Ikiwa nitachoka niiunue (Should I tire, lift me)

Refrain:
Nipe, kukumba wema (Grant me to remember good) x3
Nipe kukumba wema wako (Grant me to remember Your Goodness)

Hata kwenye bonde hili la mauti (Even in this valley of death)
Nakumbuka nilikuita, (I remember that I called)
Na wewe ukaitika Baba (And Father You answered)
Kutegemea akili zangu, na mawazo yangu (Depending on my wits and my thoughts)
Kutanifanya niendelee (Will make me continue)
niendelee kulalamika (Continue to complain)
Kuna kipindi najisahau (There are times I forget)
na kujivunia mafanikio (And boast of my achievements)
Wengine naona takataka (I see others as rubbish)
Nikumbushe mi ni mtu tu (Remind me that I am but a man)
na dunia tunapita (The world shall pass away)
Uhai wangu si faida bila wewe (My life is not profitable without You )

Mungu wewe ni mkuu (God You are greater)
kuliko vile nakutazama Baba (Than what I can fathom, Father)
Unisamehe, unisamehe (Forgive me, forgive me)
Kuna nyakati nadhani (There are times I suppose)
hii dunia labda ni ya ushindani (That this world maybe is for competition)
Natumia akili zangu za ndani (I use my inner thoughts)
Ila bado nashindwa kuendelea (Only I am unable to continue)
Nikimbushe nisidhani (Remind me not to think)
Wakifanikiwa tuna upinzani (That should they succeed, we are in opposition)
Nifundishe kuwaombea amani (Teach me to pray peace for them)
Na utatenda kwa wakati (And You will act in time)

(Na ikiwa) Kama nikisahau (Should I forget)
Unikumbushe mi mtoto wako (Remind me, your child) (Repeat)

(Refrain)

Hauwezi Kushindana (You Cannot Compete) Lyrics by Goodluck Gozbert

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Refrain:
Hauwezi kushindana, oh kushindana
(You cannot compete, cannot compete)
Na mwanadamu mwenye kinywa
(With a person with a mouth)
(Repeat)

Kama maneno yangekuwa yanaweza kutoboa mwili huu
(If words were able to pierce this body)
Mbona sasa ningekuwa na vidonda mwili mzima
(Then my body would be full of wounds)
Vita vya maneno kuna watu ni majemedari
(In the war of words, there are Generals)
Ukisema mshindane mbona mikono mtainua
(If you were to compete, you will lose)
Kupigwa vita ni kawaida isikusumbue
(Being fought is usual, do not let it bother you)
Wewe ni mti wenye matunda, zoea mawe
(You are a tree with fruits, get used to the stones)
Lia kidogo, nyamaza ili uchungu uishe
(Cry a little, then be quiet that the pain will end)
Ukiendelea unawapa kichwa hao
(When you continue, you confuse them more)
Basi laza imani, rejea vitani
(Then pick up your faith and return to the fight)
Wakikuona waseme, umekuwa sugu
(When they see you to say you have become tough)
Acha waongee, acha waseme seme
(Let them speak, let them talk about you)
Ila yuko Mungu wakuwaziba midomo
(For there is a God that will shut their mouths)

(Refrain)

Ikiwa Mungu anahukumu kwa kusikiza maneno
(If God judged by listening to words)
Mbona hata matumbo ya mimba yanasemwa sana
(Then what of pregnancies that are talked about a lot)
Hivi Mungu angehukumu kwa kusikiza umbea
(If God judged by listening to gossip)
Si ningekushauri mchungaji wangu ufunge kanisa
(Then I would advise you my minister to close the church)
Mwanadamu, mwanadamu shida ni ulimi
(The human, the man has an issue with the tongue)
Ungejifunza ukimya, haunanga hasara
(If you teach it silence, you will not lose)
Fulani, we fulani una shida gani?
(My friend, what is your problem?)
Na uongo wanini? Mwogope Mungu
(Why lie? Fear God)
Ukumbuke ni ahadi, kuna siku yaja
(Remember it is  a promise, that a day is coming)
Kwa kila neno na kinywa chako utatolea hesabu
(That every word from your mouth with be brought to account)
Mimi nimeshakwambia kubali uwache
(I have already told you, agree to leave it alone)
Utajijua na shingo yako ngumu
(You will understand yourself to be tough)
Siwezi kushindana, oh kushindana
(I cannot compete, cannot compete)
Na mwanadamu mwenye kinywa
(With a human with a mouth)

(Refrain)

Yesu, huyu Yesu hakujitetea kabisa
(Jesus, this Jesus did not defend himself)
Japo walimsema kwa ubaya aliwasamehe
(Though they talked with evil intents, He forgave them)
Na wewe uwasamehe, uwaombee
(And you forgive them, and pray for them)
Kwa maana hawayajui wasemaya
(For they do not know ..?)
Wakifingyanga ubaya, uwajibu kwa wema
(When they do wrong, answer them with kindness)
Usishindane na mtu, wajibu kwa wema
(Do not compete with anyone, answer them with kindness)
Ata iwe ni ndugu wa karibu, wajibu kwa wema
(Even if it is your close brother, answer them with kindness)
Si vizuri wewe, usilipe kisasi, wajibu kwa wema
(It is not good for you to revenge, answer them with kindness)
Tena wema uende, wajibu kwa wema
(Do good and leave, answer them with kindness)
Eh, wajibu kwa wema
(Oh, you answer with goodness)
Maana x2
(Because, because)

(Refrain)

Ipo Siku (There Is a Day) Lyrics by Goodluck Gozbert

1 Comment


(Sung in Swahili)

Ni mbali nimetoka (I’ve come from far)
Tena ni ajabu kuwa hai (And it’s amazing that I’m still alive)
Maana ningeshakufaga (For I should have died)
Ni mengi nimeona (I have seen many things)
Tena ya kuvunja moyo (Many of them heartbreaking)
Labda ningeshamwacha Mungu (That I should have left God)

Bridge:
Kama ni misongo ya mawazo (If it is pressuring thoughts)
Magonjwa mama, nimepitia, ninazoea (Or illnesses, I’ve been through, I’m used to them)
Maumivu ya kudharauliwa, umasikini (Hurt from contempt, poverty)
Ni kila siku, ninajipa moyo: (Everyday, I encourage myself:)

Refrain:
Ipo siku yangu tu, Ipo Siku (There is my day, a day)
Ipo siku yangu tu (My day)
Nami (Niba niba nibarikiwe) (That I will be blessed as well)
Nami nibarikiwe (nibarikiwe) (That I will be blessed as well)
Nibarikiwe (nibarikiwe) (I be blessed)
Nami nibarikiwe ( nibarikiwe) (I be blessed as well)
Niba, niba, nibarikiwe (I be blessed)

Ingawa kwa sasa wananisema vibaya (Though they currently speak ill of me)
Nami sishangai – najua ni ya wanadamu hayo (I am not dismayed – these are earthly things)
Ingawa sipati na ni kwa muda mrefu (Though lack for a long time)
Siachi kuomba; Mungu si kiziwi (I do not stop praying; God is not deaf)
Binadamu wema, ukiwa nacho (Men are good when you have things)
Kwa sasa waniepuka sina rafiki wa dhati (But now they avoid me, I do not have friends)

(Bridge + Refrain)

Miaka imepita, unaombaga mtoto hupati (Years are past, you’ve prayed in vain for a child)
Vuta subira maana Yeye hachelewi (Be patient, for He’s never late)
Ona biashara imeandamwa mikosi hupati (Your business is followed by misfortunes)
Usimwache Mungu, waganga watakuponza (Do not abandon God, witchcraft will destroy you)
Mpo kwa ndoa ila nyumbani amani hakuna (There is no peace in your marriage)
Msimwache Mungu – michepuko sio jibu (Do not abandon God – separation is not the answer)
Umeugua tumaini la kupona hakuna (You are terminally ill – no hope of survival)
Usimtazame mwanadamu siku yako imekaribia (Do not hope on men, your day is coming)

Najua Ayaya (Ipoa) x? (I know, itwill be well)

Misuko-suko ya ndoa (The travails of marriage)
Mtoto anakusumbua (Your child grieves you)
Giza likiingia unawaza wapi utalala (When darkness comes, you don’t know where to sleep)
Masimango Mashemeji, ati huzai mtoto (Your in-laws mock your barrenness)
Masimango mama wa kambo (Your step-mother mocks you)
Umemchosha nyumbani (She is tired of you)
Usiwaze usiumie, najua yote yatapita (Do not be discouraged, all shall pass)
Siku imekaribia, najua yote yatapita (Your day is near, I know all shall pass)

Nawe ubarikiwe (nibarikiwe) (That you should be blessed)
Ubarikiwe (nibarikiwe) (Be blessed)
Nawe ubarikiwe (nibarikiwe) (That you should be blessed)
Uba, Uba, Ubarikiweee (Be blessed)

%d bloggers like this: