Yamebadilika (Things Have Changed) Lyrics by Komando wa Yesu ft Madam Martha

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Mtakaa asubuhi, kiza kitaingia
(You will wait from morning, until darkness come)
Kusubiri aibu yangu kama mlivyozoea
(Waiting for my shame like you’re used to)
Ina maana hamjui, imebaki historia
(But you do not know, that that is now history)

Kati ya watakaofutwa machozi
(From among those whose tears would be wiped)
Nami nimechaguliwa (I have been chosen)
Kilio changu cha muda mrefu, amekisikia
(My longstanding cries, He has heard them)
Hakuna tena cha mikosi: ni kufanikiwa
(There is no more troubles: Now it is prospering)

Refrain:
Wa zamani si wa sasa (The one  of the past is not of the present)
Mambo yamebadilika, eh (Things have changed)
Imekula kwe- imekula kwenu eh (Now shame is on you)

Namjua ninayemtumikia (I know whom I serve)
Namjua ninayemwimbia (I know whom I praise)
Mfalme wa wafalme (King of kings)
Funguo ya maisha yangu (Keys of my life)

Mlinicheka sana (You laughed o much)
Mpaka kudiriki kusema (That you could not speak)
Namwamini Mungu, asiyeona (I believe in God who does not discriminate)

Na niliposema nitajenga majumba (When I said I will build houses)
Yaani, mlicheka sana (You laughed at me)
Niliposema nitamiliki magari (When I said I will drive cars)
Mkaguna “mhh, ndoto ya mchana” (You complained “Mh, daytime dreams”)
Mkasema ni ndoto, ndoto (You said it was all dreams)
Niache utoto (I should grow up)
Maana haiwezekani (Because they were impossible)

Kumbe yupo Msemaji wa Mwisho (But there is one with the final say)
Anaandaa kesho yangu (He prepares my tomorrow)
Nisibakie kama jana (For me not to remain like yesterday)
Aibu hiyo (Shame to you)

Baba yangu si kiziwi (My father is not deaf)
Hata asinisikie (That he would not listen to me)
Baba yangu si kipofu (My father is not blind)
Hata asinione (That He may not see me)
Baba yangu si mchoyo (My father is not selfish)
Hata asinibariki (That he may not bless me)
Mlipanga mabaya (You planned evil on me)
Imekula kwenu (Shame now is on you)

Wa zamani si wa sasa (The one  of the past is not of the present)
Mambo yamebadilika (Things have now changed)
Mlipanga nife (You planned for my demise)
Imekula kwenu, eh (Now shame is on you)

(Refrain)

Wa zamani si wa sasa (The one  of the past is not of the present)
Yale yaniyonitesa (What persecuted me)
Nayo yamebadilika (Now has changed)
Imekula kwenu eh (Now shame is on you)

(Refrain)

Walizoea kuona naharibikiwa (They got used to my spoilt plans)
Wakasema sitafanikiwa (They said I will not be successful)
Mungu, amebadilisha mambo (God, has changed things)

Pale akili yenu ilipoishia (Where your thoughts ended)
Baba yangu nd’o anapoanzia (That is where my Father started from)
Jambo, kufanya jambo (To do great things)

Mtakaa barazani kuniongelea (You will sit in your councils, speaking against me)
Mabaya kuniombea (Praying evil on me)
Ila ng’ambo, nitavuka ng’ambo (But I will cross over)

Kama ni kiwete nimetembea (If I was lame, I have now walked)
Aibu kaniondolea (He has removed my shame)
Mimi sio yule wa jana (I am not as I was yesterday)

(Refrain)

Tunaye Baba mwenye uweza, Alfa na Omega
(We have a father who is capable, Alpha and Omega)
Huinua wanyonge toka mavumbini machoni pa adui
(He lifts the weak from dust, in front of their enemies)

Unayenisikiliza, kipi kinakuliza?
(The one who listened to me, what is bothering you?)
Mwambie Yesu, achana na wanadamu hao
(Tell Jesus, leave those humans alone)

Hata wakuite tasa, sawa (Even if they call you barren, it is ok)
Waseme masikini, sawa (They say you are poor, it is OK)
Waseme huolewi (They said you cannot get married)
Matusi yote wamalize (Let them finish all their insults)

Wala usiwajibu, sawa (But do not respond to them, OK)
Nyamaza kimya, sawa (Be quiet, OK)
Kisasi si chako wewe (Revenge is not yours to mete)
Mambo yatabadilika (Things will change)

(Refrain)

Mimi si yule wa jana, wa sasa (I am not like yesterday)
Namuona Bwana, badilika (I have seen my Lord, and changed)
Usiku na mchana (Day and night)
imekula kwenu (Imekula kwenu eh) (Shame is on you)

Yaliyoshindikana, wa sasa (What was blocked, now is different)
Yamewezekana (All is possible)
Hata useme hapana (Even if you say no)
Imekula kwenu, imekula kwenu eh (Shame is on you)

(Refrain)

Wacha Waone (Let Them See) Lyrics by Goodluck Gozbert ft Martha Mwaipaja

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Refrain:
Wacha waone, wacha waone (Let them see, let them see)
Wacha waone, vile wewe ni ngome, Yesu (Let them see the way you are a Fortress)

Niko hapa kukuwakilisha, Yesu wangu (I am here to represent You, my Jesus)
Nataka waone vile ulivyo ngome kwangu (I want them to see the way You are my safe haven)
Tumetoka mbali, umenitoa mbali (We have come from far, You have brought me from far)
Ninaomba waone ulivyo mkubwa (I pray that they may see Your might)
Ulikonitoa  mimi najua (I know where You brought me from)
Ndio maana nasema, wewe ni mwamba (That is why I say, You are the Rock)
Sitarudi kule nilikotoka, niko na wewe (I will not return from whence I came, I am with you)
Kwangu ni mwamba (You are my Rock)
Uliko nivusha mimi najua (Where You brought me across, I know)
Ndio maana nasema, wewe ni mwamba (That is why I say, You are the Rock)
Kwa macho waone ulivyo Ili nao waelewe (Let them see with their eyes, that they may know)
Wewe ni ngome (That you are the fortress)
Kwa macho wakujue, nilie naye (With their eyes to know whom I am with)
Wao waseme kweli ni ngome (For them to confess that You are the fortress)

(Refrain)

Sibishani, sibishani na wabishi sugu (I do not argue with the stubborn)
Nisije nikasema; kakasirika Mungu (That I may speak out and anger God)
Sitetei sitetei, hali yangu ngumu (I do not defend my tough life)
Siunajua ukitenda, watatafutana huku (Because You know if You do it, they will look for You)
Eh Yahweh, sina wa kulinganisha na wewe (Oh Lord, I do not have anyone to compare to You)
Nashukuru shukuru shukuru Kyala (I am thankful to You)
Hata yale ulinitendea pasipo kuomba eh (Even to what you did for me without my prayer)
Ngome yangu ya siri: ni wewe Mungu (My secret fortress, is You, God)
Kuna vile unipigania nisiaibike eh (You fought for me, that I may be safe)

Utawale, utawale tu, utawale (Rule, rule over us)
Utawale, utawale tu, utawale (Rule over us)

(Refrain)

Katika vitu, katika watu (In all things, amongst all people)
Ukaniinua, nashukuru Yesu (You lifted me, thank You Jesus)
Katika vitu, katika watu (In all things, amongst all people)
Nikaheshimiwa, nashukuru Yesu (I have been respected, Thank You Jesus)

Repeat: Daida
Sasa najidaidai (Now I take pride)
Nafurahi rahi (I am joyful)
Asante (Thank you) (Repeat)
Nafurahi Leo (I am joyful today)
Najidai kwa Yesu (I take pride in Jesus)
Ninaendelea, ah (I continue)
Ninashangili ah (With my praise)
Kwa Baba, eh (To the Father)
Najidai, ah (I take pride)
Ninaringa kwa Baba (I take pride in the Father)
Nafurahi kwa Yahweh (I am joyful in Yahweh)

Repeat:
Jidhihirishe Mungu (Show yourself God)
Utukufu wako (In all Your Glory)
Ukitamalaki hapa, utatamalaki Bwana (Take authority Lord)

Najulikana Mbinguni (I am Known in Heaven) Lyrics by Martha Mwaipaja

1 Comment


(Sung in Swahili)

Ninajulikana mbinguni (I am known in heaven)
Ninaheshimiwa mbinguni (I am respected in heaven)
Nimehesabiwa na Yesu mwenyewe (I have been counted by Jesus Himself)
Ananitosha milele (He satisfies me forever)
Ninajulikana kwa Baba juu (I am known by Father above)
Ninaendelea tu na Yesu (I continue with Jesus)
Nimehesabiwa mbinguni juu (I have been counted by heaven on high)
Amenipenda mimi, mwokozi (The Savior loves me)

Sijajiweka mwenyewe mimi mwenzio (I have not elevated myself)
Nimewekwa na Mungu (God has placed me there)
Sijawahi jitambulisha mwenyewe (I do not brag for myself)
Nimetambulishwa na Baba (The Father brags about me)
Walisemezena tusimtambulishe huyu (While they have agreed not to recognize me)
Nimetambulishwa mbinguni (I am recognized in heaven)
Wakasema tusimchague (They said I should not be chosen)
Nimechaguliwa mbinguni (I have been chosen in heaven)
Wakasema tusimkubali (They rejected me)
Nimekubaliwa na Baba (The father welcomed me)
Nimewekwa na Mungu Mwenyewe (I have been elevated by God himself)
Najulikana Mbinguni, najulikana mbinguni (I am known in heaven, I am known in heaven)

Refrain:
Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu (I am known in heaven, I walk with Jesus)
Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu (I am known in heaven, I walk with Jesus)
Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu (I am known in heaven, I walk with Jesus)
Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu (I am known in heaven, I walk with Jesus)

Unajulikana mbinguni rafiki ndugu yangu, mbingu inakujua
(My friend and brother, you are known in heaven)
Wametangaziana wasikusaidie, umesaidiwa na Mungu
(They have told themselves not to help you, but God helps you)
Wameabikizana wasikutendee, umetendewa na Baba
(They have planned to work with you, God works with you)
Wamesama wakufute kwenye ukoo wao, umeandikishwa mbinguni
(They have agreed to remove you from the clan roster, but you are registered in heaven)
Wamekataa kukutambulisha, unatambulishwa na Mungu
(They have refused to recognize you, God recognizes you)
Walisema hawatakutibu kabisa, umeponywa na Mungu
(They said they will not treat you, but you have been healed by God)
Wamekataa kukubeba, umebebwa na Yahweh (They refused to carry You, but Yahweh carries You)
Wametamani ulie kila siku, Baba kakukumbuka (They have desired to see you cry, but the Father remembers you)
Hujui vile nilivyo pendwa na Mungu! (You have no idea how much I am loved by God!)

(Refrain)

Mhukumu wa Haki (The Just Judge) Lyrics by Martha Mwaipaja

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Parapanda itapigwa, itapigwa (The trumpet shall be sounded, it shall be sounded)
Parapanda itapigwa, itapigwa (The trumpet shall be sounded, it shall be sounded)
Parapanda itasikika, itasikika (The trumpet shall should, it shall sound)
Parapanda itasikika, itasikika (The trumpet shall should, it shall sound)

Hapo ndipo Mfalme wa haki atakapotawala
(That is when the King of Justice shall reign)
Mfalme wa kweli, atakapotawala (The true King shall reign)
Maana dunia ya leo, watu wanapendeleana
(For in today’s world, people practice favoritism)
Maana dunia ya leo, watu wanapendeleana
(For in today’s world, people practice favoritism)
Atatawala mwenye dunia (The owner of the earth shall reign)
Atatawala mwenye watu wake (He shall reign over His people)
Maana dunia ya leo, watu wanapendeleana
(For in today’s world, people practice favoritism)
Maana dunia ya leo, watu wanapendeleana
(For in today’s world, people practice favoritism)

Hapo ndipo falme zote za dunia zitasimama
(That is when all the kingdoms of the earth shall cease)
Mwenye haki ya kweli atatawala (And the just One shall reign)
Atasimamia mahakama, zote kwa haki (He shall take over all the courts with justice)
Atasimamia kesi, zote kwa haki (He shall take over all the cases with justice)
Kila mmoja atalipwa sawa (Everyone shall be treated equally)
Dunia yote itatishwa kwenye uweza wake
(The entire earth shall be amazed by His mighty)
Dunia yote itashangaa, alivyo wa haki
(The whole earth shall be astonished, with his justice)
Mataifa watajua, yeye ni mwema
(All nations shall know that He is Good)

Hapo ndipo wote tutajua kwamba yeye ni Baba
(That is when we shall know that He is the Father)
Dunia yote itaelewa, ni muhukumu wa haki
(The whole earth shall understand, He is the just Judge)
Maana dunia ya leo watu wanasaidiana
(For in today’s world, people practice favoritism)
Maana dunia ya leo watu wanasaidiana
(For in today’s world, people practice favoritism)
Atatawala asiyejua pendelea mwingine
(He shall reign, the One who does not practice favoritism)
Watu wa leo wanatazama sifa za mtu
(For people today only look at someone’s praises)

Majira yanakuja ya kujua Baba wa kweli
(The season is coming to know the True Father)
Majira yanafika, watamjua Mungu wetu
(The season is coming, they will know our God)
Leo hawatambui machozi tunayolia
(For today they do not understand our teears)
Leo hata ukilia, hakuna wa kutazama
(For today when you cry, there are no witnesses)
Hata ukiteswa, hakuna wa kutazama
(Even when you are persecuted, there are no witnesses)
Wakati unakuja, baba atatatawala kwa haki
(The time is coming, for the Father to reign in justice)
Hapo ndipo falme zitajua yeye ni Mfalme
(That is when other kingdoms would know that He is the King)
Hapo ndipo dunia itaelewa yeye ni Bwana
(That is when the world will understand that He is the Lord)
Tutapanguswa machozi yetu, na sisi (Our tears will be wiped away)
Tutapanguswa machozi yetu, na sisi (Our tears will be wiped away)
Tutaheshimiwa na dunia, na sisi (We shall be respected by the world)
Tutaheshimiwa na watu wote, na sisi (We shall be respected by every person)

Hawawezi tambua haki yako leo hii (For they will not recognize your rights today)
Maana dunia ya leo, watu wanasaidiana (For in today’s world, people practice favoritism)
Hakuna wa kutetea maisha yako (There is no one to advocate for your life)
Maana tawala za leo, wanapendeleana
(For today’s kingdoms, there is favoritism)
Anakuja mtawala wa haki, kutusaidia (The Just King is coming to help us)
Anakuja mtawala wa haki, kutusaidia (The Just King is coming to help us)

Utafurahi na Baba (You shall be glad with the Father)
Tutashangilia kwa Baba (WE shall rejoice in the Father)
Maana falme yake Baba itakuwa ni yenye haki
(For the Father’s kingdoms are righteous)
Maana falme yake Baba itakuwa ni yenye haki
(For the Father’s kingdoms are righteous)
Baba yetu atatawala (Our Father shall reign over us)

Repeat: Atatawala (He shall reign)
Atatawala Masiya (The Messiah shall reign)
Atatutawala kwa haki (He shall reign over us with justice)
Atatawala, atatulipa wote (He shall reign, and )
Ee Baba, ee Baba, Baba (Oh Father, Oh Father, Oh Father)
Atubembeleza, Baba (The Father shall comfort us)

%d bloggers like this: