Akisema Atakubariki (If He Says He Will Bless You) lyrics by Jemimah Thiong’o

1 Comment


Chorus:
Akisema atakubarik hakuna atakayezuia
(If he says He will bless you, no one will prevent it)
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote
(For He is the God with all the blessings)
Akisema atakubarik hakuna atakayezuia
(If he says He will bless you, no one will prevent it)
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote
(For He is the God with all the blessings)

Akisema atakubariki, wala usitie shaka
(If He says He will bless You, do not orry)
Kwani yeye ndiye Mungu mwenye baraka zote
(For He is the God with all the blessings)
Mipango yake ya ajabu, tena haibadiliki
(His plans are amazing, and they do not change)
Akisema atakuinua, ndiye mwenye kuinua
(If He says he will lift You, He is the lifter)
Akisema atakupa mtoto, katika umri wowote
(If He says He will give you a child, at any age)
Aliwapa Sara na Ana, lipi asiloweza
(He gave to Sarah and Hannah, What can He not do?)

(Chorus)

Akisema atakubariki, watoto wako waelimike
(If He says He will bless you, your children to be educated)
Wapate na shahada nyingi, hakuna atakayezuia
(To get a lot of degrees, no one can prevent it)
Akisema utapona, hakuna atakayezuia
(If He says you will be healed, no one can prevent it)
Mama aliyetokwa na damu alipona na kazi(?) yake
(For He healed the woman with the issue of blood)
Akisema atakubariki, hakuna atakayezuia
(If He says He will bless you, no one will prevent it)
Atalinda afya yako, maana yeye ndiye mwenye afya
(He will care for your health, for He is the one who gives it)

(Chorus)

Watembelea miguu, hata baisikeli huna
(You trek on foot, you do not own even a bicycle)
Akisema uendeshe Musso, kesho utaendesha
(If He says you will drive a Musso, tomorrow you will drive it)
Waishi nyumba ya matope, huna hata mavazi
(You live in a house made in mud, you do not even have clothing)
Akisema atakubariki, majirani watashangaa
(If He says He will bless you, even your neighbors will be amazed)
Akisema atakuinua, mbele ya adui zako
(If He says He will lift You, before your enemies)
Atakuandalia meza ule unywe wakitizama
(He will prepare a table for you to eat and drink as they look on)

(Chorus)

Amenipanda (He Has Planted Me) Lyrics by Jemimah Thiong’o

Leave a comment


Refrain:
Bwana asema, amenipanda mimi
(The Lord has said, that He has planted me)
Kando ya mito yenye maji mengi
(Near the source of many waters) (Repeat)

Ni Bwana alonipanda, kwa mikono yake Baba
(It is the Lord that has planted my with his hands)
Kando ya mito yenye rehema na baraka
(Next to the source of mercy and blessings )
Kunipalilia Baba, sikosi mbolea maji
(The Lord has weeded me, I do not lack fertilizer or water)
Naishi nikiamini, siwezi nyauka nimepandwa ee
(I live believing that I will not wither, for I have been planted)

(Refrain)

Kweli Baba wa rehema, amenipanda mimi (Truly the Lord of Mercy has planted me)
Baraka zanifuata kokote niendako (Blessings follow me wherever I go)
Amenipa uhai, akalinda afya yangu (He has given me life, and protected my health)
Ndiposa nashuhudia, sifa alozipanda Mungu wangu (This is why I testify, praising my God who has planted me)

(Refrain)

Imani ya wokovu, Hushinda majaribu
(Faith of salvation, has victory over trials)
Hiyo ni baadhi ya mito nilopandwa kwayo
(This are some of the sources of waters that I am planted to)
Mambo yangu yote baba, hupanga kwa utaratibu
(All my affairs have been deliberately planted)
Kwa maana anijali, aliyenipanda Mungu wangu wee
(For He cares for me, the God who has planted me)

(Refrain)

Hakuna juu mbinguni, wala chini duniani
(There is none in heaven, or on earth below)
Anayeshinda Mungu muumba mpanzi wangu
(That defeats God, my creator, my planter)
Hunizunguka mimi, kwa damu ya mwanao
(He surrounds me, with the Blood of His Son)
Hunilinda vyema, sipati madhara kwani nimepandwa ee
(He defends me well, I am not harmed for I have been planted)

(Refrain)

Newer Entries

%d bloggers like this: