Najivunia (I’m Proud) A Cappella by Voices

Leave a comment



(Sung in Swahili)

Najivunia, Yesu wangu (I’m proud of my Jesus)
Amenipa uwezo (He has enabled me)

Najivunia Yesu (I pride myself in Jesus)
Mwenye kunipa uwezo (the one who enables me)
(Repeat)

Najivunia Yesu Mwenye kunipa uwezo (I pride myself in Jesus who enables me)
Chini za mbawa zake, Tufani ijapo vuma (Under His wings; though the storm rages,)
Ndiwe nikiwa kweli, Ajuaye shida zangu (He is my comforter, He knows my troubes)
Najivunia Yesu wangu (I pride myself in my Jesus)

Refrain:
Wakati wa zamani sikutambua (A long time ago I didn’t know)
Kwa sababu nilikuwa gizani (Because I was in darkness)
Leo nina sababu ya kutambua (But today because of knowledge)
Amenipa uwezo, Baba (I know I am enabled by my Father)

Wakati wa zamani nilikuwa… (A long time ago I was…)
Yesu wangu akaniita kwa sauti ya upole (My Jesus called me with a soft voice)
Akanipa amani, tumaini, na uzima (He gave me peace, hope and life)
Najivunia Yesu mwenye kunipa uwezo (So now I pride myself in Jesus my Hope)

(Refrain)

Wakati wa zamani (A long time ago)
nilikuwa kwenye giza (I was in darkness)
Yesu akaniita (Jesus called me)
Kwa sauti ya upole (In a soft voice)
Yesu akanitoa kwenye giza (Jesus picked me out of the darkness)
Yesu wangu, amenipa uwezo (My Jesus, He enables me)

Nalegea (I am Frail) Lyrics By Rose Muhando

1 Comment




(Sung in Swahili)

{Nalegea, wacha nichakae nje (I am frail, let me be degenerate on the outside)
Lakini utu wangu wa ndani wa fanywa upya} (But my inside man is renewed) x2
{Dhiki yangu ni nyepesi na ya muda (My suffering are light and finite)
Yaani fani wa utukufu wa milele (But my coming glory is forever)} x2
{Nayahesabu mambo yote bure (I count all things as nothing)
Kwa ajili ya jina la Yesu (Kristo) (For the sake of the name of Jesus(Christ))} x2

{Natazama, tena imeandikwa (I look and see it has been written)
Ni mizuri kama nini – miguu yao (How beautiful are their feet)} x2
{Wale wote wapelekeo habari njema (All those who spread the good news)
Ya utukufu wa Yesu Kristo Bwana wangu (Of the glory of Jesus Christ my Lord)} x2
{Nayahesabu mambo yote kama mavi/bure (I count all things as refuse/useless)
Kwa ajili ya uzuri wa Yesu (Kristo) (For the sake of the goodness of Jesus)} x2

Vipi mwenzangu, wanitazama (Why are looking at me like that friend?)
Ninaposema habari zako (When I tell you about you)
Ninapotaja na mambo zako (When I list your actions)
Wacha Makali, hasira nyingi (Ease up, Ease your anger)
{Wazielekeza juu yangu, bila sababu (You are sending it my way for no reason)
Na kumbe mimi ni mtumishi, niliyetumwa (Yet I am but a messenger sent)} x2

Nikikwambia uache dhambi (When I tell you to leave sin)
Ushirikina, uchawi fitina (polytheism, sorcery, gossip)
Wanichukia, wanichukia (You hate me, you hate me)
{Lakini Bwana asema hivi, ni ole wenu (But the Lord say this, “Woe unto you”)
Wanawake washonao hirizi viunoni mwao (women who tie charms around their waists)
Wanaoroga kwa mafumbo, wasio na haya} (The shameless who enchant with proverbs)} x2

{Sikia, ewe mkaidi, (Listen! You stubborn one)
Ee mwenye shingo ya chuma (You with a neck made of steel)
Utavuna ulichopanda, (You shall harvest what you sowed)
Mabaya yatakupata (Evil shall find you) } x2

{Kumbuka ewe mshirikina: (Remember you who practice witchcraft)
Uzao wa mwanamke mchawi (The fruits of a witch: )
Mumeo atatwaliwa, (Your husband will be taken away)
Wanao watabaki yatima (Your children will remain orphans)
Na uchawi, hautakusaidia (Your witchcraft will not help you) } x2

{Ninawaangalia yatima, (I watch over the orphans)
Ninawafahamu wajane (I know the widows)
Nimesikia kilio  chao, (I have listened to their cries)
Nimeyaona mateso yao (I have seen their sufferings) } x2

{Lakini Yesu, amefukuka (But Jesus has risen)
Dhambi, mauti hakuna tena (Sin and death are no more)
Shetani kuzimu, anatetemeka (Satan in hell, is trembling)} x2

{Eh Halleluya, sasa twashinda (Eh Hallejah, now we win)
Mapendo yakimbia kwa jina lake (His love spreads in his name (?)) } x2

Wewe, Yesu ni njia (He you! Jesus is the way)
Wewe, Yesu ni uzima (Hey you! Jesus is life)

Nisizame (That I May Not Drown) Lyrics by Tumaini

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Chorus:
Nisizame Yesu, uniokoe (That I might not drown, save me Jesus)(x2)
NIsizame uniokoe  (Save me, that I may not drown) (x2)
(repeat)

Magonjwa yananiandama (Illnesses hound me)
Hospitali zote nimaliza (I have visited all hospitals)
Kupona sijapona (I have not received healing)
Magonjwa yananiandama (Illnesses hound me)
Madaktari wote nimemaliza (I have visited all doctors)
Kupona sijapone (I have not received healing)
Njoo haraka unisaidie, nisizame (Come quickly and save me that I may not drown)
Uje hima unikoe, nisizame (Come fast and save me, that I may not drown)

(Chorus)

Naona huduma imekuwa nzito (I see my ministry becoming heavy)
Naona huduma hii Baba yangu kama ni mzigo (I feel my ministry as a burden, Father)
Naona huduma imekuwa nzito (I fell the burden becoming heavy)
Umekuwa kama mwiba (It has become a thorn)
Lakini nakuita unisaidie, nisizame (But I call unto you to help me, that I may not drown)
Nisizame Baba, nisizame (Don’t let me drown father)

(Chorus)

Elimu nimemaliza (I have completed my education)
Kazi nimetafuta, nimekosa (Looked for work, to no avail)
Mwenye nymba naye amekukuja (The landlord has come)
Akidai kodi ya nyumba  (He wants the rent for the house)
Hata shilingi mimi sina (And here I am penniless)
Nimejaribu kuomba kwa majirani (I have tried borrowing from neighbors)
Ndugu zangu wote hakuna msaada (From my brothers, there’s no help)
Marafiki zangu, hakuna msaada (From my friends, there’s no help)
Ni wewe tu msaada wangu, nisizame (You are my only hope, that I may not drown)
Hili ni ombi langu, nisizame (This is my prayer, that I may not drown)

(Chorus)

Wakuabudiwa (You Deserve to be Worshiped) Lyrics by Christina Shusho

16 Comments


(Sung in Swahili)

Refrain:
Wakuabudiwa, wakuheshimiwa ni wewe Mungu (You are worthy of worship and Honor)
Wakupewa sifa, na utukufu, ni wewe Mungu (worthy to receive all praise and glory)
Mungu mwenye nguvu, wastahili heshima zote (Mighty God, you deserve all honor)
Hakuna mwingine wa kulinganishwa na wewe Mungu (There’s no one like you God)
(Repeat)

Umesema wewe, jina lako liko liliko ni we Mungu (You’re the I AM God)
Unafanya mambo yaliyo juu ya fahamu zetu Mungu (You do amazing things God)
Ukisema ndiyo, nani awezaye kupinga? Hakuna (If you say yes, no one can say no)
Wewe unatupa kushinda na zaidi ya kushinda (You give us victory over victory)
Unatupandisha utukufu hadi utukufu; Mungu (You lift us from glory to glory God)

(Refrain)

Uzima wetu uko mikononi mwako Mungu (Our lives are in your hand God)
Unawapa nguvu, wanyonge na wadhaifu Mungu (You give strength to the weak God)
Unawanyeshea mvua wema na waovu mungu (You rain on the good and the evil God)
Wanadamu nani wa kulinganishwa na wewe (Who is man to be compared to you?)
Nani mwenye nguvu wa kusimama mbele yako Mungu (Who can stand before you ?)

Post
Bwana utukufu wako sigusi (Father I do not touch your glory)
Bali utukufu ukurudie wewe Mungu wangu (But let the glory return to you my God)

Utukuzwe (Be Praised) Lyrics by Rose Muhando

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Ee Mungu utukuzwe, milele na milele (Oh God be praised forevermore)
Tena uinuliwe, katika mataifa yote (And be lifted up in all nations)
Ee Mungu utukuzwe, milele na milele (Oh God be praised forevermore)
Ee Mungu uinuliwe, milele na milele (Oh God be lifted forevermore)
Tena uhimidiwe katika mataifa yote (And be worshiped in all nations)
Jina lako la ajabu, Wewe utishaye kuliko (Your awesome name; terrifies than a lion) x2
Wala haufanananishwi na chochote (You cannot be compared with anything else)
Jina lako Baba la ajabu (Lord, your name is awesome)

Refrain:
Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika) (You hit a rock, and water sprang forth)
Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia) (In the desert, you opened a way)
Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania) (When confronted, you fought for them)
Wakafika (Kule Kanaani salama) (You led them safely to Canaan) (Repeat)
Usifiwe, utukuzwe (Be praised, be magnified) (x2)
Utukufu ni wako, milele na milele (All glory belongs to you forevermore)(Repeat)

Haya visiwa na viimbe (Let the seas sing)
Mito na ipige makofi (The rivers to clap in praise)
Ndege na waseme amina kubwa (The birds to say a big amen)
Wanyama wa mwitu wasifu (The wild animals to praise) (Repeat)

Bwana anatawala/Maana unatawala, wewe Bwana(The Lord reigns, you Lord)
Heshima na enzi ni vya Bwana (Honor and dominion are the Lord’s)
Utukufu na nguvu ni vya Bwana (Glory and Might are the Lord’s)
Umeketi mkono wenye nguvu (You who sit on the mighty hand) (Repeat)

(Refrain)

Heshima ni yako (milele na milele) (All honor is yours, forevermore)
Utukufu ni wako (milele na milele) (All glory is yours, forevermore)
Heshima ni yako (milele na milele) (All honor is yours, forevermore)
Mamlaka ina wewe (milele na milele) (Dominion is yours, forevermore)
Malaika waimbe (milele na milele) (Let the angels sing, forevermore)
Wazee ishirini na nne waseme (milele na milele) (And the 24 elders say, forevermore)
Na wale wenye uhai waimbe (milele na milele) (Let all the living sing, forevermore)
Na watakatifu waseme (milele na milele) (And all the Holy to say, forevermore)

(Refrain)

Older Entries Newer Entries