Mke Mwema (A Virtuous Wife) Lyrics by Bonny Mwaitege

Leave a comment


Hapo mwanzo mungu alimwumba Adamu (In the beginning God created Adam)
Bustani ya edeni aitunze (To care for the Garden of Eden)
Baadaye Mungu aliona sio vyema(Then God saw that it was not good)
Adamu awe pekee yake akampa mke mwema(For Adam to be alone, He gave him a wife)
Hapo mwanzooo(In the beginning)

Chorus:
Mke mwema anatoka kwa Bwana(A virtous wife is from the Lord)
Nimemwomba Mungu nangojea(I have asked God, I am waiting) (x2)
Mke mwema aaa (A virtuous wife…)

Kwa akili zangu ni vigumu kutambua (On my own it is hard to determine)
ni nani aliyeumbwa kwa ajili yangu(Who was created for me)
Katika mabinti wengi ni nani(In the midst of all the women, who is it)
Mungu ndiye anajua mke mwema(It is only God knows who)

(Chorus)

Majukumu yananizidi jamani nachoka
Kazi za ndani haziishi mke sina
Majukumu yananizidi jamani nachoka
Kazi za ndani haziishi kazi sina
Nimeshapika deki, Nguo zangu zote chafu
Nimemaliza kufua, vyombo vyote ndani vichafu
Maharage yanaungulia, ndani maji nimeishiwa
Nimeamini mwanaume bila mke hajakamilika
Nimeamini mwanaume bila mke hajakamilika bado

(Chorus)

Ukitafuta chumba cha kupanga kama hujaoa
Unaweza kuzunguka mpaka ukachoka
Ukitafuta chumba cha kupanga kama hujaoa
Unaweza kuzunguka mpaka ukachoka
Kila nyumba unayokwenda unaambiwa
“Vyumba viko, umeoa? kama hujaoa kaka samahani
Hapa hatupangishi vijana ambao bado hawajaoa.” Oh!

(Chorus)

Jina La Yesu (The Name of Jesus) by Marion Shako

Leave a comment


(Sung in Swahili)

Nalijua jina moja, jina lenye thamani (I know one name, one precious name)
Nalijua jina moja, jina lenye thamani (I know one name, one precious name)
Nalijua jina moja, jina lenye thamani (I know one name, one precious name)
Nalijua jina moja, jina lenye thamani (I know one name, one precious name)

Chorus:
Naliita jina la Yesu,yawe ngome imara (I call upon the name of Jesus, to be my solid rock)
Mwenye haki hukimbilia,Naye akawa salama (The righteous run to him, and they are safe)
Naliita jina la Yesu,yawe ngome imara (I call upon the name of Jesus, to be my solid rock)
Mwenye haki hukimbilia,Naye akawa salama (The righteous run to him, and they are safe)

Najua utamu wa hili jina,Nilimwita akaniokoa (I know how sweet the name is, I called and he saved me)
Najua utamu wa hili jina,Nilimwita akaniokoa (I know how sweet the name is, I called and he saved me)
Najua utamu wa hili jina,Nilimwita akaniokoa(I know how sweet the name is, I called and he saved me)
Najua utamu wa hili jina,Nilimwita akaniokoa(I know how sweet the name is, I called and he saved me)

(Chorus)

Wanyonge waliita, wenye haki waliinua (The weak called to him, the righteous lifted it in praise)
Jina hili ni ngome imara, kwa yule anayeliita (This name is a solid rock, to whoever calls to it)
Wanyonge waliita, wenye haki waliinua (The weak called to him, the righteous lifted it in praise)
Jina hili ni ngome imara, kwa yule anayeliita (This name is a solid rock, to whoever calls to it)

(Chorus)

Hafungi Macho lyrics by Willy, Daddy Owen and Danco

1 Comment


Refrain:
Mungu Baba yeye hafungi macho (God the father does not sleep)
Habadiliki jana leo na kesho (He does not change, yesterday, today and tomorrow)
Azijua raha na shida zako (He Knows your joy and your sorrows)

Macho yake makali yaona mambo yote (His sharp eyes sees everything)
Hata yale yamefichika anaona (Even the unseen he sees)
Hana jambo la siri asioliona (There is no secret he does not see)
Umekosa chakula mavazi hata pesa (You don’t have food clothing and even money)
Kodi ya nyumba karo ya shule hata mchumba (Your rent, school fees even a beau)
Unadhani sasa dunia imefika mwisho (You think the world is coming to an end)

(Refrain)

Jirani, wacha mirungirungi, rafiki wacha maneno mengi
(Neighbor, abandon your worries, My friend, abandon your words)
Sijui kwa nini wanisema, Eti mimi, nimekuwa kafiri
(I don’t understand why you gossip, that I am a hypocrite)
Eti mimi nimekuwa mrui, sijui, wala sisemi kitu
(That I am a backslider, I don’t know, but I am silent)

(Refrain)

Akisema yuakuona jamani usitie shaka (If he says he sees you, please do not worry)
Ye halali na hachoki na wala ye habadiliki (he does not sleep he does not tire nor does he change)
Azijua raha zako, azijua na shida zako (He knows your joy, he knows your sorrows)
Tuimbeni halleluya Hossanah ye amefufuka (Let us sing Haleluyah, Hossana he is risen)
Haleluyah, ye halali na hachoki na wala ye habadiliki (Haleluya, he does not sleep, he does not tire nor does he change)
Haleluyah, tuimbeni haleluya Hossana ye amefufuka (Haleluya, let us sing haleluya hosanna he is risen)

(Refrain)

Kunywa Maji Lyrics by Joan Wairimu

Leave a comment


Verse 1:

Yesu kamwambia, mwanamke msamaria kisimani
Hao wanaume ulio nao hawamalizi kiu, kunywa maji
Ee dada kunywa maji, kunywa maji
Kwani ukinywa haya hamna kiu tena
Minisketi hipster fashioni Hazimalizi kiu kunywa maji

Chorus

Kunywa maji, Kunywa maji,
Kunywa maji, ya uzima

Verse 2:

Mzee mbona kiu, na maji yapo, Kila siku pombe, sigara mdomoni
Leo ni atoti, kesho ni wanjiku, Watakumaliza kunywa maji
Kijana nakwambia usidanganyike, Raha za dunia, hazimalizi kiu
Madawa ya kulevya na dot komu, Hazimalizi kiu kunywa maji

(Chorus)

Verse 3:

Ee mama Kunywa maji uache fitina,
Wivu masengenyo na mashindano
Maji ya uzima, furaha tele
Kila siku mama ni haleluya

(Chorus)

Wacha pombe, Kunywa maji ya uzima

(Chorus)

Ugali Sosa Lyrics by Man Ingwe

Leave a comment


Chorus:

Natafuta ufalme wa Mungu na utakatifu wake
Na vitu vyote vile vizuri, nitaongezewa kama ugali sosa
Huwezi pewa ugali sosa kama bado hujanunua
Basi mwenzangu mtafute Mungu, utaongezewa ugali sosa

Verse 1:

Kuna hoteli ambayo mi huenda, kukamata ugali na supu ya magoti
Mara tu mlima wa ugali ukifika, naanza kufanya test za mluhya
Ya kwanza nafinya ugali, inachomoka pande zote za mkono
Ya pili navumba ugali tupa kwa ukuta, narudi kama tennis
Ya tatu napuliza ugali, na moshi nyeupe inaenda spiral
Ugali inapata certificate, waiter leta sosa

(Chorus)

Verse 2:

Naanza kusakata ugali, namega ugali hapo kwa ngotitsa
Halafu namwona wepukhulu, kumbe alikuwa upande ule wa meza
Waiter anamkaribia anamwuliza nikupe nini Bwana
Wepukhulu anasema, ugali sosa na kadhalika
Waiter anasema excuse me? Wepukhulu anazusha
Mabouncer wakambeba juu, wakamtandika, chonga viazi

(Chorus)

Verse 3:

Sasa wasee iko hivi, tabia mbaya lazima tutawacha
Tunataka baraka zake Mungu, lakini tunakataa Mungu mwenye baraka
Tunataka tupate uponyaji lakini tunakataa Yesu mwenye kuponya
Tunapenda sana miujiza lakini hatumpendi Mungu mwenye kutenda
Ni lazima tutatubu wapendwa, tubadili mienendo tumtafute Mungu
Ukidharau mambo hii nasema, haki roho safi utachonga viazi

Older Entries Newer Entries