Huniachi (You Won’t Leave Me) Lyrics By Reuben Kigame Ft. Gloria Muliro

3 Comments


(Sung in Swahili)

Refrain:
Umeahidi wewe Bwana huniachi
(Lord You have promised never to leave me)
Hadi mwisho wa dahari(?) ulisema, huniachi
(Even until the end of Age you said You will never leave me)
Wewe ni Mungu uliye mwaminifu, siku zote
(You are a faithful God, all the time)
Mimi ninaiweka imani yangu kwako Baba
(I’ve put my faith in You Father)

Nipitiapo maji mengi au moto, huniachi
(When I go through many waters or fire, you’ll never leave me)
Unalijua jina langu ewe Bwana, huniachi
(Lord You know my name, You’ll never leave me)
Unatengeneza njia hata mito, kule jangwani
(You’ve prepared a way and streams in the wilderness)
Wewe ndiwe Alfa na Omenga, huniachi
(You are the Alpha and Omega, you’ll never leave me)

(Refrain)

Uliwalinda Waisiraeli kule jangwani
(You protected the Israelites in the wilderness)
Ukamtoa Danieli kutoka tundu la simba
(You saved Daniel from the Lion’s den)
Wewe huwainua na wanyonge, siku zote
(You uplift the weak, all the time)
Watuepusha na hatari kila siku, usifiwe!
(You keep us from danger every day, Be praised!)

(Refrain)

Baba hata mama wanaweza kunipaga
(My father and mother may betray me)
Marafiki nao wanaweza nigeuka
(My friends can turn their backs on me)
Mara kwa mara maadui wanizunguka
(Time and again my enemies surround me)
Nitaishi kwa ahadi yako Bwana, Huniachi
(I will live in your promise Lord, never to leave me)

(Refrain)

Advertisement

Fadhili Zake ni Za Milele (His love Endures Forever) By Reuben Kigame & Sifa Voices

3 Comments


(Sung in Swahili)

Zaburi 136; tumshukuru Bwana na tuimbe pamoja (Psalm 136 – Let us thank the Lord and sing together)

Chorus:
Mshukuruni Bwana, (Give thanks to the Lord)
Kwa kuwa ni mwema (For He is good)
Kwa maana fadhili zake (For His mercies)
Ni za milele (Endures forever)

Refrain: Fadhili zake ni za milele (His love endures forever)

Mshukuruni Mungu wa miungu (Thank the God of gods)
Mshukuruni Bwana wa mabwana (Thank the Lord of lords)
Amefanya maajabu (He has done great things)
Yeye alifanya mbingu na nchi (He created the heavens and the earth)
Sema Kabisa (Say it loud)

(Chorus)

Amefanya mianga mikubwa (He created great lights)
Jua litawale mchana (The sun to rule by day)
Mwezi na nyota usiku (The moon and stars by night)
Akatandaza nchi juu ya maji (He laid the earth over waters)
Imba kabisa (Sing out loud)

(Chorus)

Aliyeigawa Bahari ya Shamu (He who divided the Red Sea)
Akavusha Waisiraeli (And ferried the Israelites)
Aliyemshinda Farao (He who defeated Pharaoh)
Na majeshi yake yote (And all His armies)
Sema kabisa (Say it aloud)

(Chorus)

Yeye aliyetukumbuka (He who remembered us)
Katika unyonge wetu (In our weakness)
Atuokoaye na watesi (He who saves us from adversaries)
Mungu kweli ni wa ajabu (God truly is awesome)

(Chorus)

Enda Nasi (Go With Us) Lyrics by Reuben Kigame with Sifa Voices

21 Comments


(Sung in Swahili)

Tunaomba uwepo wako uende nasi (We pray for your presence to go with us )
Ewe Bwana wa majeshi utusikie (Oh Lord of Hosts, listen to us)
Kama huendi nasi, hatutaki kutoka hapa (If you won’t go with us, we don’t want to leave)
Hatuwezi pekee yetu, enda nasi ( We can’t by ourselves, go with us)

Tu watu wa shingo ngumu tusamehe (We are a stubborn people, forgive us )
Hatufai mbele zako, turehemu ( We are undeserving, redeem us)
Tusafishe ee Baba, tuonyeshe uso wako (Cleanse us Father, show us your face )
Twahitaji neema yako, enda nasi (We need your grace,  )

Chorus:
Tutavua mapambo yetu, (We shall remove our ornaments )
Vitu vyote vya thamani kwetu (Everything  we value )
Mioyo yetu twaleta mbele zako (Our hearts we bring before you  )
Tutakase na utembee nasi (Cleanse  us and walk with us)

Tunaomba utuonyeshe njia zako (We pray that you show us your ways  )
Kwa maana umetuita kwa jina ( For you have called us by your name )
Twalilia Ee Bwana, utukufu na uso wako (We cry for your glory and your face Oh Lord)
Bila wewe tutashindwa, enda nasi (Without you Lord we shall be defeated, go with us )

(Chorus)

Sina Mungu Mwingine (I Have No Other God) Lyrics by Reuben Kigame and Sifa Voices

7 Comments(Sung in Swahili)

Pre-Song:
Oh Baba, mimi sina Mungu mwingine nimfahamuye (Oh Father, I don’t know any other God) Ni wewe pekee ujazaye Roho yangu (You alone fill my spirit)

Verse 1:
Sina Mungu mwingine, wa kutegemea (I don’t have any other God to depend on)
Mbinguni na duniani, hapana mwingine (Heaven and earth, there is no other)
Sina cha kupendeza, wala cha faida (I have nothing pleasing, or profitable)
Ila wewe Bwana wangu, Mungu wa milele (Only you my Lord, Everlasting God)

Verse 2:
Mwili na moyo wangu, vyaweza zimia (My body and heart may fail)
Bali Mungu ndiye mungu wa uhai wangu (But God is the God of my life)
Yeye sehemu yangu, milele daima (He is my portion forever)
Nitaingia hema yake, na sifa zake kuu (I shall enter his tent with praise)

Chorus:
Ni nani mwingine, ajazaye roho yangu (Who else fills my spirit)
Na kunipa raha kamili (And gives me full joy)
Ni nani semeni, akomboaye mwanadamu (Tell me who else saves man)
Na kumshindia shetani (and defeats the devil on his behalf?)

(Verse 1) + (Chorus)

Baba Yetu (Our Father) by Taifa Mziki Choir Lyrics by Reuben Kigame

2 Comments(Reuben Kigame’s Version)

(Sung in Swahili)

Verse 1:
Baba yetu wa mbinguni tunaleta sifa kwako
(Our Father in heaven we bring praises to you)
Wewe hulinganishwi na yeyote duniani
(You cannot be compared to anyone in the world)
Mbingu na nchi zakusifu, jua na mwezi vyakutukuza
(Heaven and earth praise you, the sun and the moon worship you)
Wanyama wa pori, ndege wa angani (Wild animals, birds of the air)
Sifa tele kwako Bwana (Multitudes of praises to you Lord)

Mbingu na nchi zakusifu, jua na mwezi vyakutukuza
(Heaven and earth praise you, the sun and the moon worship you)
Wanyama wa pori, ndege wa angani (Wild animals, birds of the air)
Sifa tele kwako Bwana (Multitudes of praises to you Lord)
(Repeat)

Chorus: *Hoiye is a sound (of praise)
Hoiye! Sifa zetu, Hoiye! ni zako zote
(Hoiye, Our praises belong to you alone)
Hoiye! Usifiwe, Hoiye! Milele Bwana
(Hoiye be praised forever Lord) Repeat

Verse 2:
Tukiomba kwako Baba, sikio lako li wazi kwetu
(When we pray to you Father, your ears are open to us)
Macho yako yatuona; sisi watoto wako
(Your eyes see us; your children)
Ulimtoa Yesu, mwana wako wa pekee
(You gave your only son Jesus)
Alikufa msalabani; sasa tuko huru
(To die on the cross; and now we are free)

Newer Entries

%d bloggers like this: