Najivunia, Yesu wangu (I’m proud of my Jesus)
Amenipa uwezo (He has enabled me)
Najivunia Yesu (I pride myself in Jesus)
Mwenye kunipa uwezo (the one who enables me) (Repeat)
Najivunia Yesu Mwenye kunipa uwezo (I pride myself in Jesus who enables me)
Chini za mbawa zake, Tufani ijapo vuma (Under His wings; though the storm rages,)
Ndiwe nikiwa kweli, Ajuaye shida zangu (He is my comforter, He knows my troubes)
Najivunia Yesu wangu (I pride myself in my Jesus)
Refrain:
Wakati wa zamani sikutambua (A long time ago I didn’t know)
Kwa sababu nilikuwa gizani (Because I was in darkness)
Leo nina sababu ya kutambua (But today because of knowledge)
Amenipa uwezo, Baba (I know I am enabled by my Father)
Wakati wa zamani nilikuwa… (A long time ago I was…)
Yesu wangu akaniita kwa sauti ya upole (My Jesus called me with a soft voice)
Akanipa amani, tumaini, na uzima (He gave me peace, hope and life)
Najivunia Yesu mwenye kunipa uwezo (So now I pride myself in Jesus my Hope)
(Refrain)
Wakati wa zamani (A long time ago)
nilikuwa kwenye giza (I was in darkness)
Yesu akaniita (Jesus called me)
Kwa sauti ya upole (In a soft voice)
Yesu akanitoa kwenye giza (Jesus picked me out of the darkness)
Yesu wangu, amenipa uwezo (My Jesus, He enables me)
Kamba za mauti zilinizunguka mie (The chains of death surrounded me)
Mafuriko ya maovu yakanitia hofu (The flood of evil made me afraid)
Kamba za mauti zilinizunguka mie (The chains of death surrounded me)
Mitego ya mauti ikanikaribia mimi (The trap of death neared me)
Niliona shida,Niliona taabu (I saw trouble, I saw suffering)
Nikakuita Bwana wangu na wewe ukaitika (I called you my Lord, and you answered)
Kumuacha Bwana sio kuzuri Baba/Mama yangu (Leaving Him is not good dad/mum) x2
Nilimuacha mimi, nilipata shida/taabu (I left Him and suffered/troubled) x2 (Repeat)
Nikakimbia kimbia kwake Yesu/Baba (So I ran to Jesus/Father) x2
Parapanda ya Bwana ii karibu (The Lord’s trumpet is near)
Parapanda karibu kusikika (The trumpet shall be heard soon)
Wazima wote watasikia (All who live shall hear it)
Na waliokufa wote wafufuke (Those who are dead shall rise)
Walomsubiri watavikwa taji zilizong’aa (Those who waited for Him will be crowned)
Bali waovu wataukimbia uso wake (But the evil shall flee His face)
Refrain:
Tutamwona mfalme wetu Yesu, akirudi (We shall see our kings’ return)
Tutafurahi, tupumzike, wote tuloshinda (We’ll rejoice and rest all who’ve conquered)
Nao malaika wote, wapige panda (The angels shall sound the trumpets)
Nyingi za ushindi (With resounding joy)
Na tutaruka mawinguni (And we shall rejoice in the clouds)
Tumlaki mfalme wetu (While meeting our King)
Watakaokuwa ni washindi, Watafurahia ajabu (The winners shall rejoice)
Na majina yao yataitwa, Naye Yesu mwokozi wao (Their names called by Jesus their savior)
Wataruka kwa furaha angani (They shall jump for joy in the air)
Wakiongozwa naye Yesu (Led by Jesus)
Nyimbo tamu zitasikika angani (Sweet songs shall be heard)
Ndugu yangu usikose pale (My brother, do not miss it)
Utakuwa wapi siku hiyo ndugu? (Where will you be on that day?)
Utakuwa wapi siku hiyo? (Where will you be on that day?)
Mwokozi Yesu atakapoyaita (When our Savior Jesus shall call)
Majina yao aliowakomboa (The names of all He has saved)
Walio ya furaha mavazi katika damu ya Yesu (The ones who wear garments washed with His blood)
Wakavumilia hadi kufika mwisho (Those who persevered to the end)
Refrain:
Ni kwanini umeyaruhusu, (Why have you permitted)
Ee Mungu mwenyezi (Oh God Almighty)
Yatusononeshe moyoni (For our hearts to be troubled)
Kwanini unaruhusu (Why have you permitted it?)
Ona haya machozi; Tazama tunavyolia (Look at these tears; how we weep)
Twajiuliza sana Bwana (We ask ourselves Lord)
Ni kwanini uliyaruhusu (Why you permitted it)
Nikumbukapo usiku huo (When I remember that night)
Usiku wa huzuni nyingi (A night filled with sorrow)
Ulipokubali Bwana kwamba (When you permitted Lord)
Wenzetu wapumzike (That our friends should rest)
Najiuliza moyoni, (I ask in my heart)
Kwanini Bwana Mwenyezi (Why, Oh God almighty)
umeruhusu tusononeshwe kiasi (You’ve allowed us to suffer thus?)
(Refrain)
Mlipuko ni ghafla (An explosion is sudden)
Tulipovamiwa na mauti (When we were invaded by death)
Bwana ulimruhusu ndugu Gautane (Lord you allowed Gautane)
Aiage dunia (To leave the world)
Ndugu Amosi, Mansi kijana mnyenyekevu (Brother Amos, Mansi a humble brother)
Twawakumbuka wote – hatutawasahau (We remember them all – we shall not forget them)
(Refrain)
Twahuzunika Bwana, tena nawe wajua (We mourn Lord, you know this)
Lakini kwa hayo yote (But for all that)
Chukuliwa kwa matendo mema (Be lifted by your great works)
Uliyoyakubali wale watumishi wako (That you allowed your servants)
Wayatende katika siku hizo (To do in those days)
Chache za maisha (Those few days of their lives)
Twayakumbuka matendo yenu (We remember your works)
Mema yasiyoelezeka (The good works that cannot be counted)
Mliotena duniani (That you did while in the world)
Twawakumbuka tulivyoishi vizuri (We remember how we lived well)
Kwa muda mlikuwa nasi; hatutawasahau (In the time you were with us – we won’t forget) (Repeat)