Nyoosha Mkono Wako (Stretch Out Your Hand) Lyrics by Msanii Music Group

1 Comment

(Sung in Swahili)

Kila siku twazidi kuwa wapotovu (Everyday we are corrupted)
Kwamba maadili Mungu alivyoagiza (By the standards God imparted us)
Tunatamani kuwa wakamilifu (We desire to be as perfect)
Kama mitume wa zamani (Like the apostles of old) (Repeat)

Refrain:
Nyoosha mkono wako, tufani zavuma (Stretch out Your hands, thunderstorms are intense)
Tuma malaika wako, tupe nguvu zako (Send Your angels to grant us Your strength)
Sisi tu wenye dhambi, Bwana turehemu (We are sinners, have mercy upon us)
Nyoosha mkono wako, tuweze kushinda (Stretch out Your hand, that we may win)
Nyoosha mkono wako, tuweze kushinda (Stretch out Your hand, that we may win) (Repeat)

Ulinzi wako uwe pamoja nasi (May Your protection surround us)
Ili tuweze kushinda majaribu (That we may overcome temptations)
Hatua kwa hatua, utupe ushindi( Step by step, grant us victory)
Tuongoze katika haki (Lead us into righteousness) (Repeat)

(Refrain)

Pengine Milimani (Perhaps to the Mountains) Lyrics Sung by Msanii Music Group

Leave a comment

(Sung in Swahili)

Refrain:
Pengine milimani, utanituma niende (Perhaps You will send me to the mountains)
Pengine mabondeni, wataka nipeleke neno (Perhaps You intend for me to preach in the valleys)
Dhahiri sitakataa, wito wake Bwana Mungu (Certainly I will not refuse the call of the Lord God)
Niko hapa, nitume niende leo! (Here I am, send me today!)

Bwana ninaomba, hivi leo uniongezee nguvu (Lord I pray, that You increase my strength today)
Kwa maana sijui wataka niende wapi (For I do not know where You intend for me to go)
Ili jambo moja ni hakika, wala kamwe sina shaka (But one thing I know, and I will never doubt)
Unanitaka niende, nikahubiri neno lako (You want me to go and spread Your Gospel)
Unanitaka niende, nikahubiri neno lako (You intend for me to go and preach Your Word)

(Refrain)

Kwanza nitaanza hapa hapa kwa majirani zangu (I will begin right here with my neighbors)
Kwani nuru hii lazima, kwanza iangaze karibu (For this light must shine close)
Na ndipo hatua kwa hatua, shinde nitasonga mbele (And then step by step I will move forwards)
Kadri uniwezeshavyo, nilipeleke neno lako (According to how You enable me to spread Your Word)
Kadri uniwezeshavyo, nilipeleke neno lako (According to how You enable me to spread Your Word)

(Refrain)

Hakuna Gumu Kwako (Nothing is Impossible to You) Lyrics by John Lisu

Leave a comment

(Sung is Swahili)

Wewe ndiwe Mungu (You are God)
Wastahili utukufu (You deserve the praise)
Umefanya mengi ya ajabu (For You have done amazing things)
We ni mfalme (You are the King)

Refrain:
Hakuna gumu kwako, Yesu (Nothing is impossible to You, Jesus)
Hakuna gumu kwako (Nothing is impossible to You)
Hakuna gumu kwako Yesu (Nothing is impossible to You, Jesus)
Hakuna gumu kwako (Nothing is impossible to You)

Ulitembea juu ya maji, Yesu (Nothing is impossible to You, Jesus)
Hakuna gumu kwako (Nothing is impossible to You)
Wafanya njia pasipo na njia (You make a way where there is no way)
Hakuna gumu kwako (Nothing is impossible to You)

Na wagonjwa wanapona, Yesu (You heal the sick, Jesus)
Hakuna gumu kwako (Nothing is impossible to You)
Hakuna gumu kwako Yesu (Nothing is impossible to You, Jesus)
Hakuna gumu kwako (Nothing is impossible to You)

(Refrain)

Kuta za gereza zatingizika (The prison walls are shaken)
Minyororo yakatika (The chains are broken)
Wafungwa wafunguliwa, Yesu (The prisoners are released, Jesus)
Hakuna gumu kwako (Nothing is impossible to You)

(Refrain)

Mashtaka yetu yamefutwa (The accusation)
Vita vyetu ni juu ya Bwana (Our battles belong to the Lord)
Falme zitainuka, falme zitaanguka (Kingdoms will rise and fall)
Bali ufalme wako wadumu (But Your Kingdom is everlasting)

Falme zitainuka, falme zitaanguka (Kingdoms will rise and fall)
Bali ufalme wako wadumu (But Your Kingdom is everlasting)

(Refrain)

Milima yayeyuka kama nta ,mbele zako (Mountains melt like wax before You)
Wanguruma kama rad,i wewe Mungu mwenye nguvu (You roar like thunder, You are a mighty God)
Uliumba pasipo wewe kuumbwa (You created but not were not created)
Wewe ni Mfalme (You are King) (Repeat)

Msalabani (On the Cross) Lyrics by Neema Gospel Choir (AICT Chang’ombe)

Leave a comment

(Sung in Swahili)

Msalabani pa Mwokozi (At the Savior’s Cross)
Wapatikaana ukombozi (We find redemption)
Ni kazi ya thamani yake Yesu (It’s the precious work of Jesus)
Msalabani pa Mwokozi (At the Savior’s Cross) (Repeat)

Tumesamehewa dhambi hatuna deni (Our sins have been pardoned, we have no more debt)
Amelipa yote Bwana hatuna deni (The Lord paid it all, we have no more debt)
Ni kazi ya thamani yake Yesu (It is the precious work of Jesus)
Msalabani pa Mwokozi (At the cross of our savior)(Repeat)

Unyenyekevu, uvumilivu, na upendo (Humility, perseverance, and love)
Huruma nyingi na fadhili kwetu (His abundant Goodness and Mercy upon us)
Ni sifa za thamani zake Yesu (It’s the precious attribute of Jesus)
Msalabani pa Mwokozi (At the Savior’s Cross) (Repeat)

Tumesamehewa dhambi hatuna deni (Our sins have been pardoned, we have no more debt)
Amelipa yote Bwana hatuna deni (The Lord paid it all, we have no more debt)
Ni kazi ya thamani yake Yesu (It is the precious work of Jesus)
Msalabani pa Mwokozi (At the cross of our savior)(Repeat)

Ni kazi ya thamani yake Yesu (It is the precious work of Jesus)
Msalabani pa Mwokozi (At the cross of our savior)

Sioshwi Dhambi (What Can Wash Away Sins) Hymn Lyrics Sung by Diakonias Gospel Team

Leave a comment

(Sung in Swahili – A Hymn)

Refrain:
Hakuna kabisa (There is nothing)
Dawa ya makosa (The cure of sin)
Ya kututakasa (To cleanse us)
Ila damu ya Yesu (But the Blood of Jesus) (Repeat)

Sioshwi dhambi zangu (What can wash away my sin?)
Bila damu yake Yesu (Nothing but the blood of Jesus)
Hapendezewi Mungu (What can me whole again?)
Bila damu yake Yesu (Nothing but the blood of Jesus)

(Refrain)

La kunisafi sina (For my cleansing this I see)
Ila damu yake Yesu (Nothing but the blood of Jesus)
Wala udhuru tena (For my pardon this my plea)
Ila damu yake Yesu (Nothing but the blood of Jesus)

(Refrain)

Sipati patanishwa (Nothing can for sin atone)
Bila damu yake Yesu (Nothing but the blood of Jesus)
Hukumu yanitisha (Naught of good that I have done)
Bila damu yake Yesu (Nothing but the blood of Jesus)

(Refrain)

Sipati tumaini (This is my hope and peace)
Bila damu yake Yesu (Nothing but the blood of Jesus)
Wema wala amani (This is all my righteousness)
Bila damu yake Yesu (Nothing but the blood of Jesus)

(Refrain)

Yashinda ulimwengu (It conquers the world)
Hiyo damu yake Yesu (That blood of Jesus)
Na kutufikisha juu (And gets us to heaven)
Hiyo damu yake Yesu (That blood of Jesus)

(Refrain)

Older Entries Newer Entries