Nyota ya Ajabu lyrics by Rose Muhando

3 Comments

ILe nyota ya ajabu, yaonekana mashariki
Imejaa ishara zote, za kuzaliwa mfalme
Mamajuzi wako nyuma, kuifuata nyota ile
walifika Yerusalemu, nao wakauliza (repeat)
Yuko wapi yeye aliyezaliwa,
mtawala wa wayahaudi ili tumsujudie

Chorus:
Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi
Atakayewaokoa watu na dhambi zao
Dunia shangilieni, amezaliwa messiah
Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana

Walikuwako na wachungaji, waliokaa makondeni
Wakilinda kundi lao kwa zamu usiku
Malaika kawatokea, kawambia msiogope
Maana leo katika Yuda, amezaliwa messiah

(Chorus)

Walipokwisha kusema haya, Malaika wa bwana
Waliimba wimbo ule, wimbo usio na mwisho
Utukufu juu kwa Mungu mbinguni
Duniani we amani kwa aliowaridhia

(chorus)

Maongeo enzi yake, na tena begani mwake
Tazameni anakuja kwa jina lake Bwana
Maongeo enzi yake, na tena begani mwake
Tazameni anakuja kwa jina lake Bwana

(chorus)

Sitanyamaza Lyrics by Rose Muhando

2 Comments

(Sung in Swahili)
Eeeehhhh…. Mimi Mungu (Me, God)
Matendo nitalia, Kwa sinani nitaomboleza
Sodoma nitanung’unika, Mipakani nitashambulia
Mijini wameniacha,Kila mara nitashambulia
Maisha ya wanadamu, Yamenichosha….

Oh oh mimi
Sitanyamaza, wala sitanyamaza
Lakini nitalipa ujira wa vifuani mwao
Maovu yenu ninyi, pamoja na baba zenu
nasema nitalipa ndio mjue mimi ni Bwana
Mmefukiza uvumba, na kunitukana
Kwa ajili ya haya mtajutia vitani mwenu?(repeat)

mmefanya uzinzi katikati ya milima
Usiku wa manane mmefanya ukahaba
Kwenye njia kuu na vichochoro mmefanya mapatano
Kwenye mialoni na mipera mmefanya machukizo (repeat)

Ulitumaini uzuri wako ukafanya ukahaba
Kila kijana aliyepita ulimwona anafaa
Awe mzuri na sura mbaya ulifunua marinda

Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi mapenzi zako mbona sasa unakonda
Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi waelizamu (?) wako mbona sasa unakonda

Miji mizuri imekuwa ukiwa
Majumba mazuri yamefungwa kabisa
Wana wa wana wamebaki yatima
Kiburi chamuwamu(?) imekoma kabisa (repeat)

Hebu sasa piga kelele uliye kahaba,
Shika kinubi omboleza upate kukumbukwa (repeat)

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye
Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)

Lakini Bwana asema hivi, nitawaponya
Yeye mwenyewe aahidi, nitawabariki
Mimi ni alfa na omega, mwanzo na mwisho
Jamani mimi ni mungu, mwingine hapana

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)

Yesu Jemedari lyrics by Wangeci Mbogo

Leave a comment

(Sung in Swahili)

Yesu ndiye Jemedari wangu
Ni jemedari wangu, hakuna mwingine
Yesu ndiye Jemedari wangu
Ni jemedari wangu, hakuna mwingine

Chorus:
Huyu yesu, Asifiwe yesu
Asifiwe yesu, hakuna mwingine
Huyu yesu, Asifiwe yesu
Asifiwe yesu, hakuna mwingine

Yesu ndiye kiongozi wangu
Anionyesha njia, popote niendapo
Yesu ndiye kiongozi wangu
Anionyesha njia, popote niendapo

(Chorus)

Yesu ndiye mwokozi wangu
Kamwaga damu yake, nipate wokovu
Yesu ndiye mwokozi wangu
Kamwaga damu yake, nipate wokovu

(Chorus)

Ahh Yesu, Yesu, huyu yesu, huyu yesu, yesu
Yesu, huyu yesu, huyu yesu, yesu
Yesu, huyu yesu, huyu yesu, yesu
Yesu, huyu yesu, huyu yesu, yesu
Asifiwe yesu, asifiwe yesu, hakuna mwingine

(Chorus)

Apewe Sifa lyrics by Wangeci Mbogo

1 Comment

mba, mba, mba, mba, mba, mba, mba, mba
mba, mba, mba, mba, mba, mba, mba, mba

Bwana wa mabwana apewe sifa, Bwana wa mabwana apewe sifa
Bwana wa mbinguni apewe sifa,Bwana wa mbinguni apewe sifa
Yeye ni mfalme apewe sifa, Yeye ni mfalme apewe sifa
Yesu mwokozi apewe sifa, Yesu mwokozi apewe sifa,

Atupenda, atujali, abariki,yeye ni mwema
Mwamba wetu, kimbilio, mfariji yeye ni mungu

Aliteseka kwa ajili yetu, Aliteseka kwa ajili yetu
Akatufia msalabani, Akatufia msalabani
Ili tupate wokovu kwake, Ili tupate wokovu kwake
Tuwe na ushindi kwa jina lake, Tuwe na ushindi kwa jina lake

Tumsifu, tumwabudu, tumwiuen, yeye ni Bwana
Jehovah Jireh, Jehovah shammah, Jehovah rafa, yeye ni Mungu

Bwana wa mabwana apewe sifa, Bwana wa mabwana apewe sifa
Bwana wa mbinguni apewe sifa,Bwana wa mbinguni apewe sifa
Yeye ni mfalme apewe sifa, Yeye ni mfalme apewe sifa
Yesu mwokozi apewe sifa, Yesu mwokozi apewe sifa,

Atupenda, atujali, abariki,yeye ni mwema
Mwamba wetu, kimbilio, mfariji yeye ni mungu
Tumsifu, tumwabudu, tumwinue, yeye ni Bwana

Newer Entries